Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mimba zisizotarajiwa, ukeketaji na unyanyasaji mwingine wa kijinsia huenda vikaongezeka wakati janga la COVID-19 linapoendelea-UNFPA

UNFPA yatarajia ongezeko la kesi za mimba zisizotarajiwa, ukeketaji na unyanyasaji wa kijinsia zitakazo tokana na janga hili la COVID-19
© UNFPA Myanmar/Yenny Gamming
UNFPA yatarajia ongezeko la kesi za mimba zisizotarajiwa, ukeketaji na unyanyasaji wa kijinsia zitakazo tokana na janga hili la COVID-19

Mimba zisizotarajiwa, ukeketaji na unyanyasaji mwingine wa kijinsia huenda vikaongezeka wakati janga la COVID-19 linapoendelea-UNFPA

Wanawake

Wakati janga la COVID-19 likiendelea, idadi ya wanawake ambao hawawezi kupata upangaji wa uzazi, wanakabiliwa na ujauzito usiopangwa, ukatili wa kijinsia na mazoea mengine mabaya yanaweza kuongezeka kwa mamilioni katika miezi ijayo, kulingana na takwimu ziliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA.

Utafiti unaangazia kiwango kikubwa cha athari ambayo COVID-19 inazo kwa wanawake wakati mifumo ya afya inapozidiwa, vituo kufungwa au kutoa huduma chache kwa wanawake na wasichana, na wengi huamua kuruka uchunguzi muhimu wa matibabu kwa kuhofia kuambukizwa virusi. Kuparaganyika kwa mnyororo wa usambazaji na ununuzi ulimwenguni unaweza pia kusababisha uhaba mkubwa wa dawa za mpango wa uzazi uzazi na unyanyasaji wa kijinsia unatarajiwa kuongezeka kadiri wanawake wanakwama nyumbani kwa muda mrefu.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Natalia Kanem, anasema, “takwimu hii mpya inaonesha athari ya janga ambayo COVID-19 inaweza kuwa nayo hivi karibuni kwa wanawake na wasichana ulimwenguni. Ugonjwa huo unazidisha kukosekana kwa usawa, na mamilioni ya wanawake na wasichana sasa wako hatarini kupoteza uwezo wa kupanga familia zao na kulinda miili yao na afya zao. Afya ya uzazi na haki za wanawake lazima zilindwe kwa gharama yoyote. Huduma lazima ziendelee; vifaa lazima kutolewa; na walio hatarini lazima walindwe na kuungwa mkono.”

Wanawake wanaofanya kazi ya kufikisha mafunzo kwa wanawake wasema wanahofia wanawake wenzao ambao wanakaa manyumbani bila kwenda popote wakati huu wa janga la corona.
© UNFPA Syria
Wanawake wanaofanya kazi ya kufikisha mafunzo kwa wanawake wasema wanahofia wanawake wenzao ambao wanakaa manyumbani bila kwenda popote wakati huu wa janga la corona.

Makisio makuu

Wanawake milioni 47 katika nchi 114 zenye kipato cha chini na cha kati wanaweza kukosa kupata uzazi wa mpango wa kisasa na ujauzito milioni 7 usiopangwa unatarajiwa kutokea ikiwa amri ya kuendelea kusalia nyumbani itaendelea kwa miezi 6 na kukatokea usumbufu mkubwa kwa huduma za afya. Kwa kila miezi 3 ya kuendelea kubaki nyumbani itakayoongezeka, wanawake milioni 2 wanaoweza kushindwa kutumia uzazi wa mpango wa kisasa.

Viza milioni 31 vya ziada vya unyanyasaji wa kijinsia vinaweza kutarajiwa kutokea ikiwa amri ya kuendelea kubaki nyumbani itaendelea kwa angalau miezi sita. Kwa kila miezi 3 ya watu kubaki nyumbani, visa vya ziada milioni 15 vya unyanyasaji wa kijinsia vinatarajiwa.

Kwa sababu ya kuvurugika kwa programu za kuzuia ukeketaji kutokana na kujikita katika kupambana na  COVID-19, visa milioni 2 vya ukeketaji vinaweza kutokea katika muongo mwingine ujao ambao ungeweza kuwa visa hivyo vimefutika.

COVID-19 itasumbua juhudi za kumaliza ndoa za watoto, pengine kusababisha ndoa za watoto milioni 13 hufanyika kati ya mwaka huu 2020 na 2030, matukio ambayo yangeweza kuwa yameachwa.