Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa amani: Kuanzia kusaidia nchi kuondoka katika migogoro, na sasa COVID-19

Walinda amani wa MONUSCO wakishiriki katika kutoa matibabu na lishe nchini DRC
UN Photo/Michael Ali
Walinda amani wa MONUSCO wakishiriki katika kutoa matibabu na lishe nchini DRC

Ulinzi wa amani: Kuanzia kusaidia nchi kuondoka katika migogoro, na sasa COVID-19

Msaada wa Kibinadamu

Kama ilivyo kwingine kote duniani, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanakabiliana na changamoto zinazoletwa na mlipuko wa virusi vya corona, COVID-19. Lakini kazi yao inaendelea na wanaendelea kutekeleza majukumu yao muhimu ya amani na usalama.

mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika idara ya operesheni za amani, Bwana Jean-Pierre Lacroix, "operesheni za ulinzi wa amani zinapaswa kuendelea na kazi yake muhimu na kuendeleza uwezo wa utendaji ili waweze kufanikisha jukumu letu la uokoaji wa maisha, kuhimiza utatuzi wa migogoro na kusaidia kulinda watu ambao tunawahudumia, wakiwemo maafisa wa Umoja wa Mataifa.” 

Sambamba na wito wa Katibu Mkuu wa kusitisha mapigano ya haraka ulimwenguni, shughuli za kulinda amani zinahimiza pande zote zilizoko katika mgogoro 'kunyamazisha bunduki', kuwezesha ufikiaji wa misaada ya kibinadamu na kujitolea juhudi zao katika kuzuia kuenea kwa coronavirus">COVID-19.

Ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa umeweka hatua kadhaa za dharura kuzuia kuenea kwa COVID miongoni mwa wafanyakazi wake na kuhakikisha kuwa walinda amani hawaambukizwi na pia kupunguza athari mbaya ya COVID-19 dhidi ya uwezo wa ulinzi wa amani kutekeleza majukumu waliyopangiwa.  

Hatua hizo ni pamoja na kufanya kazi kwa ukaribu na mamlaka za kitaifa na kuweka sera na taratibu kwa wafanyakazi wote sambamba na ushauri wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.
  
“Kwa kushirikiana na mamalaka za nchi, Tumeongeza kwa haraka hatua za tahadhari ikiwemo karantini kwa wafanyakazi wapya wanaoijunga nasi.” Amesem bwana Lacroix.

Sambamba na mambo yote, walinda amani wamekuwa wakifanya kila liwezekenalo kutumia rasilimali walizoanazo kusaidia mamlaka za nchi ili kupambana na virus.

Mathalani ujumbe wa pamoja kati ya Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID wametoa vifaa kama vile majenereta huko Darfur Kaskazini kama njia ya mpango wa kudhibiti COVID-19.

Mapema wiki hii, Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL ulichangia barakoa, glovu na mavazi ya kujikinga katika manispaa ya Naqouara huko Lebanon wanakohudumu.

Walinda amani wanaohudumu huko Mali, MINUSMA nao wamesaidia sana huko Mali katika maandalizi ya uchaguzi wa wabunge huku walinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC nao wiki iliyopita wakiwasaidia wananchi 38 wakiwemo wanawake na watoto ambao walikuwa wametekwa na makundi yenye silaha katika maeneo ya mashariki mwa nchi. 

Zaidi ya wanajeshi, polisi na raia 95,000 wametumwa kote katika operesheni 13 za Umoja wa Mataifa duniani.