Mlinda amani wa UN auawa nchini Lebanon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesikitishwa sana na kifo cha askari wa kikosi cha kulinda amani cha Ireland kutoka mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL aliyeuawa katika tukio lililotokea hapo jana tarehe 14 Disemba katika eneo la Al-Aqbieh, nje ya eneo la operesheni la UNIFIL. huko Lebanon Kusini.