Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na COVID-19 mamilioni bado wahitaji misaada- OCHA

Kambi ya Kafr Lousin Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria. Watu kama hawa, pamoja na mapambano dhidi ya COVID-19 bado wanahitaji misaada ya mahitaji mengine.
UNOCHA
Kambi ya Kafr Lousin Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria. Watu kama hawa, pamoja na mapambano dhidi ya COVID-19 bado wanahitaji misaada ya mahitaji mengine.

Pamoja na COVID-19 mamilioni bado wahitaji misaada- OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya dharura, OCHA imekumbusha kuwa mamilioni ya watu walio hatarini bado wanategemea misaada ya kuokoa maisha inayotolewa na Umoja wa Mataifa.

 

Naibu Msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo.

Bwana Laerke amesema kuwa baadhi ya nchi zilizokumbwa na virusi vya Corona au COVID-19 zilikuwa tayari kwenye janga la kibinadamu kutoka na vita, majanga ya asili na mabasiliko ya tabianchi.

Ameema ni muhimu sana kuendeleza kazi za kuokoa maisha katika hizo nchi na kwamba “tunaendeleza kazi za kibinadamu duniani kote.”

Kwa mujibu wa Bwana Laerke, “timu ya OCHA mjini Geneva zinasaidia uratibu, usambazaji wa taarifa na vifaa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu na mashinani OCHA inasaidia nchi ambazo tayari zimekumbwa au zinaweza kukumbwa na COVID-19.”

Amesema ni muhimu sana kutomwacha yeyote nyuma katika janga la sasa na kwamba lazima kushirikiana kuishinda Corona.

Wakati huu ambapo bara la Ulaya ni kitovu cha COVID-19, “kila nchi bila kujali chochote lazima ichukue hatua za kijasiri kukomesha au kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona” amesema Hans Kluge, Mkuu wa WHO barani Ulaya.