Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na kujitenga na kufunga shule tuongeze juhudi za upimaji COVID-19:WHO

Vifaa tiba vilivyotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP vikiwasili, Beijing.
Picha kwa hisani ya Yingshi Zhang
Vifaa tiba vilivyotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP vikiwasili, Beijing.

Pamoja na kujitenga na kufunga shule tuongeze juhudi za upimaji COVID-19:WHO

Afya

Wakati virusi vya corona vikiendelea kusambaa sehemu mbalimbali duniani na kuongeza idadi ya vifo, shirika la afya ulimwenguni WHO linasema huu ni wakati wa kuongeza kasi ya upimaji.

Katika taarifa yake ya leo  Jumatatu  kwa waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi kuhusu COVID-19 mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus amesema “tumeshuhudia hatua mbalimbali zikichukuliwa ikiwemo kujitenga, kufunga shule, kufuta matukio ya michezo n ahata mikusanyiko, lakini hatujashuhudia hatua za kutosha za katika upimaji, kuwaweka watu sehemu maalum na kufuatia waliokutana na wagonjwa kitu ambacho ni cha muhimu sana katika kukabiliana na maambukizi.”

Ameongeza kuwa hatua za kujitenga na matukio ya mikusanyiko ya kijamii kutasaidia kupunguza maambukizi na kuiwezesha mifumo ya afya kukabiliana na hali. Na pia unaweza kuwalinda wengine kujilinda mwenyewe kwa kuhakikisha unanawa mikono mara kwa mar ana kuziba mdomo wakati wa kukohoa.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hatua hizo pekee hazitoshi kumaliza mlipuko huu ni mchanganyiko wa hatua ndio unaoleta mabadiliko.  “Kama ninavyoendelea kusisitiza kwamba nchi zote zinapaswa kuchukua mtazamo wa kina wa hatua, lakini njia bora Zaidi ya kuzuia maambukizi na kuokoa maisha ni kuvunja mnyororo wa maambukizi  na ili kufanikisha hilo ni lazima upime na kutenga watu. Huwezi kupambana na ugonjwa huu kama hujui nani ameambukizwa”.

Watu wanaowasili kwenye uwanja wa ndege wa Luxor nchini Misri wakifanyiwa uchunguzi kupima dalili za virusi vya corona.
Khaled Abdul Wahab
Watu wanaowasili kwenye uwanja wa ndege wa Luxor nchini Misri wakifanyiwa uchunguzi kupima dalili za virusi vya corona.

Ujumbe kwa nchi zote

Dkt. Tedross ametoa ujumbe kwa nchi zote akisema “pima, pima, pima , pima kila kisa kinachoshukiwa” na kuongeza kuwa endapo watabaina wana virusi hivyo , wasi watenganisheni na wengine na mwasake wale wote waliokutana nao kwa hadi siku mbili kabla ya kuanza kuonyesha dalili nao wapimwe pia.

Hadi kufikia sasa WHO imeshasafirisha vifaa vya upimaji milioni 1.5 kwa nchi 120. “tunashirikiana kwa karibu na makampuni ili kuongeza upatikanaji wa vipimo hivyo kwa wale wanaovihitaji zaidi” ameongeza mkurugenzi huyo wa WHO.

WHO pia imeshauri kwamba visa vyote hata ambavyo si vya hali mbaya kutenganishwa na wengine katika vituo maalum vya afya ili kuzuia maambukizi na kuwexza kuwapa huduma inayostahili. Hata hivyo Dkt. Tedross amesema WHO inatambua kwamba tayari kuna nchi ambazo zimeshazidiwa uwezo na hivyo imesema “Katika hali hiyo basin chi zitoe kipaumbele kwa wagonjwa wazee na wale wenye matatizo ya kiafya ya muda mrefu.”

Kila hatua inasaidia

Kwa mujibu wa shirika hilo kuna baadhi ya nchi ambazo tayari zinatumia viwanja vya michezo, vituo vya mazoezi ya viungo ili kuwahudumia wagonjwa ambao hawana hali mbaya san ana walio mahututi ndio wanaotibiwa hospitali.

Imesema njia nyingine inayoweza kusaidia ni kwa wagonjwa ambao sio mahututi kupatiwa huduma wakiwa wametengwa majumbani kwao.

Shirika hilo limeonya kwamba “watu walioathirika na COVID-19 bado wanaweza kuambukiza wengine hata baada ya kutohisi kuumwa, hivyo hatua za kujikinga zinapaswa kuendelea kwa takribani wiki mbili baada ya dalili kutoweka.

Shirika la mpango wa chakula duniani lawasilisha vifaa tiba Hubei, China
Yingshi Zhang
Shirika la mpango wa chakula duniani lawasilisha vifaa tiba Hubei, China

 

WFP yatoa msaada wa vifaa tiba China

Wakati huohuo shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo limetoa vifaa tiba vya thamani dola 500,000 ili kuisaidia hospitali ya Hubei nchini China katika kusaidia juhudi za serikali kupambana na virusi vya Corona, COVID-19.

Akizungumzia msaada huo mkurugenzi wa WFP nchini China Sixi Qu amesema “WFP inafanyakazi kwa karibu na serikali ya China ili kuhakikisha kwamba msaada unakwenda sanjari na vipaumbele vya serikali.

Miongoni mwa vifaa tiba hivyo ni pamoja na Oksijeni, vifaa vya kupumua kwa ajili ya wagonjwa mahututi. Duruy a kwanza yam ashine 50 iliwasili jana Jumapili mjini Beijing na leo imewasilishwa kwenye shirikisho la Hubei tayari kusafirishwa hadi Wuhan ambako vinatarajiwa kuwasili Jumatano Machi 18.

TAGS:COVID-19, coronavirus,Virusi vya Corona, WFP, WHO, China