Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagonjwa wa Corona duniani sasa wavuka 153,000, Tanzania nayo imo

Waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee na watoto wa nchi hiyo Ummy Mwalimu akizungumza na Flora Nducha wa UN News kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikao cha 63
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya
Waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee na watoto wa nchi hiyo Ummy Mwalimu akizungumza na Flora Nducha wa UN News kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikao cha 63

Wagonjwa wa Corona duniani sasa wavuka 153,000, Tanzania nayo imo

Afya

Idadi ya wagonjwa wa Corona duniani ikivuka 153,000,  wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika taarifa yao iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi wamezitaka nchi kuepuka kutumia mbinu za kudhibiti mlipuko zinazokandamiza haki za binadamu.

Taarifa hiyo ya watalaamu inakuja katika kipindi ambacho nchi zinachukua hatua mbalimbali kujaribu kudhibiti maambukizi ambayo hadi kufikia sasa yamesababisha vifo 5735 na taarifa za shirika la afya duniani WHO zikionesha kuwa kuna wagonjwa wapya 10,982 duniani kote.

Nchi zikiendelea kutoa mwenendo wa mapambano, Tanzania, nchi iliyoko Afrika Mashariki imetangaza kuwa na mgonjwa wa corona.

 Tangazo limetolewa na Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu

(Sauti ya Ummy Mwalimu)

Kisha waziri Ummy anathibitisha matokeo ya uchunguzi baada ya mgonjwa huyo kufanyiwa vipimo vya kitabibu