Uganda yaimarisha juhudi za kudhibiti nzige

10 Februari 2020

Serikali ya Uganda inafanya juu chini kudhibiti nzige amabo tayari wamevamia maeneo ya kaskazini mashari mwa nchini hiyo.  Imekuwa chonjo tangu nzige hao wasogelee mpaka wake na Kenya. 

Baada ya kutangaza rasmi uvamizi wa nzige katika wilaya za Amudati, Abilatuk na Nakapiripiriti katika eneo la wafugaji wa Kikaramajong hiyo jana, hali ya panda-shuka ikijumwisha mikutano ya dharura ilianza.

Ndege mbili za kijeshi zimeonekana kwenye uwanja wa ndege wa Kololo jijini Kampala zikikata mawingu kuelekea wilayani Amudati baada ya kusheheni vifaa na dawa za kupuliza nzige kutoka angani.

Aggrey Bagire waziri wa kilimo ametaja uvamizi huu kuwa ni janga kubwa lakini akisema, ana matumaini kuwa watadhibitiwa.

CLIP:

Na kueleza utayari wa kifedha.

CLIP:

Tayari kuna ndege mbili wilayani Amudati kutoka shirika la Afirca Mashriki la kudhbiti nzige wa jangwani ambazokazi yake ni kupiliza dawa hizo kutoka angani.

Waziri Mkuu wa Uganda Dr. Ruhakana Rugunda amesema tayari serikali ya Uganda imechangia dola milioni tatu za Kimerekani ambazo ni akribu sawa na shilingi bilioni 11 za Uganda katika Shirika la kudhibiti nzige wa jangwani la Africa Mashariki (DLCO-EA). 

Amewataka wananchi kushirikiana na maafisa wa serikali pamoja na wanajeshi kukabiliana na tatizo hilo la nzige.

Tayari wametatiza kilimo na ufugaji katika nchi jirani ya Kenya na kuigharibu mamilioni ya dola kuwadhibiti.

Nzige walimalizia kuvamia Uganda mwaka wa 1995 na pia walipitia maeneo haya-haya na kunishia maeneo ya Ziwa Albert ambalo wenyeji wanalitambua kama Miwtanzige – neno la Kinyoro linalomaanisha ‘muua nzige’.

Hii ina maana kwamba maeneo yaliohatarini zaidi kuvamiwa ni yale ya mpakani na Sudani Kusini, na Jamhuri ya Kidemokrasai ya Congo, DRC na vile vile nchi hizo mbili.

Shirika na chakula na kilimo (FAO) linaonya juu ya baa la njaa huku likiziomba serikali za nchi zilizovamiwa kujitahidi kuwadhibi na madhara yake kwa uhakika wa chakula.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter