nzige

Nzige wa jangwani wawa tishio, kuna hofu ya kurejea tena Kenya

Wimbi la kizazi kipya cha nzige wa jangwani linatishia mbinu za kujipatia kipato wakulima na wafuaji, halikadhalika uhakika wa kupata chakula kwenye eneo la pembe ya Afrika na Yamen licha ya juhudi kubwa za shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na wadau wake.
 

Baa la nzige wa jangwani ni mwiba juu ya kidonda kwa wakulima na wafugaji Yemen

Maisha ya wakulima na wafanyakazi yameendelea kupata pigo kubwa kutokana na janga linaloendelea la nzige nchini Yemen ambao wamesambaratisha mazao, malisho ya mifugo na kuongeza shinikizo kwa maelfu ya watu ambao tayari wamechoshwa na miaka ya vita vinavyoendelea nchini humo limesema shirika la c

Sauti -
2'39"

02 Novemba 2020

Ungana na Flora Nduca kupata habari, makala na mashinani

Sauti -
13'6"

Janga la nzige laendelea kuzusha zahma kubwa kwa wakulima na wafugaji Yemen:FAO 

Maisha ya wakulima na wafanyakazi yameendelea kupata pigo kubwa kutokana na janga linaloendelea la nzige nchini Yemen ambao wamesambaratisha mazao, malisho ya mifugo na kuongeza shinikizo kwa maelfu ya watu ambao tayari wamechoshwa na miaka ya vita vinavyoendelea nchini humo limesema shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO.

Mlipuko wa nzige Kusini mwa Afrika watishia uhakika wa chakula:FAO 

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO leo limeonya kwamba mlipuko wa nzige uliozuka Kusini mwa afrika unatishia uhakika wa chakula na limetaka hatua zichukulie haraka kuzuia janga kubwa la kibinadamu na kunusuru mamilioni ya watu Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe. 

Ziwa Turkana hatarini kukauka, uhai wa wanaolitegemea mashakani 

Nchini Kenya, ziwa Turkana ambalo ni ziwa kubwa la kudumu lililoko jangwani liko hatarini kukauka na hivyo kutishia uhai wa watu zaidi ya 300,000 wanaotegemea kipato chao kutokana na maji yake.

Nzige wa jangwani watishia upatikanaji wa chakula Turkana nchini Kenya

Nzige vamizi wa jangwani wakiendelea kuharibu mazao kwenye kaunti ya Turkana nchini Kenya, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa,

Sauti -
2'13"

Tishio la nzige Kenya bado ni kubwa lazima kuchukua tahadhari:FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema kwa kushirikiana na serikali ya Kenya wamepiga hatua kubwa kudhibiti nzige waliovamia kaunti 29 mwezi Februari mwaka huu na sasa ni kaunti chache tu ikiwemo Turkana ambazo bado zina tatizo. Lakini limeonya kwamba kubweteka itakuwa ni hatari kubwa ya kurejea kwa nzige hao. 

Kenya imejitahidi kudhibiti nzige lakini tishio bado lipo Afrika Mashariki:FAO

Kenya imepiga hatua kubwa katika kudhibiti nzige wa jangwani ambao walivamia eneo la Afrika Mashariki mapema na kwingineko mwezi February na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazao ilioweka maisha ya mamilioni ya watu njiapanda hasa katika suala la uhakika wa chakula limesema shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO.

03 JUNE 2020

Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa,siku ya baiskeli duniani tutausikia wito wa mwendesha baiskeli.
-Guterres amesema kwamba Corona ni janga la ziada kwa wakimbizi na wahamiaji, tuchukue hatua upya.

Sauti -
13'