Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2019 unashikilia rekodi ya joto kali duniani baada ya 2016:WMO

Mwaka 2019 ilirekodiwa kama mwaka wa pili wenye joto zaidi baada ya mwaka 2016, kulingana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
WMO/Jordi Anon
Mwaka 2019 ilirekodiwa kama mwaka wa pili wenye joto zaidi baada ya mwaka 2016, kulingana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Mwaka 2019 unashikilia rekodi ya joto kali duniani baada ya 2016:WMO

Tabianchi na mazingira

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO leo limesema mwaka 1029 unashikilia rekodi ya pili ya kuwa wenye joto Zaidi duniani ukiacha mwaka 2016.

Tangazo la leo limefuatia tathimini ya kina ya ahali ya joto kwa mwaka 2019 na WMO inasema wastani wa joto katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015-2019) na miaka kumi iliyopita (2010-2019) vipindi na viwango vya joto vilikuwa vya juu katika historia.

Tangu miaka ya 1980 kila muongo umekuwa wa joto Kali kuliko uliotangulia. Na mwenendo huu unatarajiwa kuendelea kwa sababu ya ogezeko la joto hewani linalotokana na gesi ya viwandani

Takwimu zilizokusanywa

Kwa mujibu wa wastani wa seti za takwimu zilizokusanywa na kutumiwa kutoa tathimini hii kiwango cha joto cha kimataifa kwa mwaka 2919 kilikuwa nyuzi joto 1.1°C zaidi ya kiwango cha wastani kilichokuwa katika ya miaka 1850-1900, ambacho ndio kilitimika kuelezea wastani wa kiwango cha joto katika nyakati za kabla ya mapinduzi ya viwanda.

WMO inasema Mwaka 2016 kunasalia kuwa ndio mwaka uliokuwa kiwango cha juu zaidi cha joto katika historia kwa sababu ya mchanganyiko wa matukio makubwa ya El Niño ambayo huwa yanaambatana na wimbi la joto Kali na mabadiliko ya mda mrefu ya tabianchi.”

Katibu mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema “Wastani wa kiwango cha joto duniani umeongezeka kwa takribani nyuzi joto 1.1°C tangu nyakati za kabla ya mapinduzi ya viwanda na kiwango cha joto baharini kimefikia rekodi ya juu zaidi. Na kwa mwenezo wa sasa wa utoaji wa hewa chafuzi ya ukaa tunaelekea kwenye ongezeko la joto la nyuzi joto 3°C  hadi 5°C ifikapo mwisho wa karne hii.”

Mkuu huyo wa WMO amesema viwango vya joto ni sehemu tu ya hadithi hii . Mwaka uliopita na muongo uliopita imeelezewa kuwa ni ya kuyeyuka kwa barafu, kuongezeka kwa kiwango cha kina cha baharí, ongrzeko la joto baharini, ongezeko la tindikali kwenye maji na majira mabaya ya hali ya hewa.

Shirika hilo linasema haya yote yamesababaisha athari mbaya kwa afya ya ustawi wa binadamu na mazingira. “Mwaka 2020 umeanzia pale ulipoachoia mwaka 2019 kwa matukio mabaya ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi. Australia ilishuhudia mwaka wenye joto kupindukia na kwenye ukame wa hali ya juu 2019 na kuwa mfano wa moto mkubwa wa nyika ambao uliathiri watu, mali zao, wanayama pori, mfumo wa maisha na mazingira “ amesema Bwana. Taalas.