Milima mirefu zaidi duniani kuanzia Andes hadi Alps na ukanda wa milima Himalaya-Hindu Kush na Tibet hadi maeneo ya kitropiki imeathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi na athari hizo sasa zinashuka chini kwenye baadhi ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu duniani.