Antarctic yavunja rekodi ya kiwango kikubwa cha joto nyuzi joto 18.3C

Mtazamo wa angani ya barafu inayoyeyuka kwenye Kisiwa cha King George, Antarctica
UN Photo/Eskinder Debebe)
Mtazamo wa angani ya barafu inayoyeyuka kwenye Kisiwa cha King George, Antarctica

Antarctic yavunja rekodi ya kiwango kikubwa cha joto nyuzi joto 18.3C

Tabianchi na mazingira

Hofu mpya ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika sayari dunia imechochewa na thibitisho la shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kwamba Antarctic imeshuhudia viwango vya rekodi  mpya ya joto Kali ambalo limepindukia zaidi ya nyuzi 18C . 

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswis msemaji wa WMO

Clare Nullis amesema rekodi hiyo mpya ya joto iliyobainika kazikazini mwa ncha ya dunia inachukuliwa si hali ya kawaida hata katika miezi ya jua na joto kali ya majira ya kiangazi.

“Kituo cha utafiti cha Argentina kiitwacho Esperanza kilichoko kwenye ncha ya Antarctic kimeorodhesha viwango hivyo vipya vya joto jana ambalo limefikia nyuzi joto 18.3C, ambacho sio kiwango unachoweza kukishuhudiua hata wakati wa kianzi. Kiwango hiki kinapita rekodi ya byuma ya nyuzi joto 17.5C, iliyowekwa mwaka 2015.” 

Hatua inayofuata

Sasa wataalam wa WMO watathibitisha rasmi endapo kiwango hicho cha joto ni rekodi mpya kwa bara la Antactic ambalo WMO inasema watu wasilichanganye na ukanda wa Antactic ambao uko kila mahali Kusini ya latitudi 60 na ambako kirekodi ya nyuzi joto 19.8C iliwekwa katika kisiwa cha Signy Januari 1982. 

Wataalam wa WMO wanatarajiwa kutathimini mazingira ya kitabiri ya tukio hilo hususan endapo linahusiana na hali ya hewa ijulikanayo kama "foehn",  ambayo ni kawaida katika maisha ya ukanda wa Alpine , hali ambayo huambatana na upepo mkali na ongezeko la joto kutokea milimani ikielekea mabondeni au kwenye vilele vya milima hali inayosababishwa na tofauti kubwa katika msukumo wa hewa.

Bi Nullis amesema “Ni miongoni mwa eneo linaloongezeka joto kwa kasi duniani. Tunasikia sana kuhusu Arctic lakini sehemu hii ya rasi ya Antarctic inapata joto haraka sana. Kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita imeongezeka joto kwa nyuzi joto 3C. Pia kiwango cha barafu kinachopotea kila mwaka Antarctic kimeongezeka takriban mara sita kati ya mwaka 1079 na 2017.” 

Kiwango hiki kikubwa cha barafu kinayeyuka wakati barafu hiyo inayeyuka kuanzia chini kutokana na maji ya baharí kuwa na joto Kali.

Eneo lililoathirika zaidi

Kwa mujibu wa WMO kuyeyuka kwa barafu kutokea zaidi kwenye Antarctica Magharibi na kwa kiwango kidogo kwenye mwambao wa rasi na Antarctica Mashariki.

Ikija katika upande kwa kujeyuka kwa theluji Bi. Nullis ameonya kwamba karibu asilimia 87 ya theluji kwenye pwani ya rasi ya Antarctic imepungua katika miaka 50 iliyopita na kasi imeongezeka zaidi katika miaka 12 iliyopita.

Amesema hofu ni kubwa hususani kwa theluji Magharibi mwa Antárctica  hasa hasa kwenye kisiwa cha theluji cha Alpine ambako migawanyiko miwili ya theluji kubwa ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza mapema mwaka 2019 sasa imekuwa na kufikia urefu wa kilometa 20.