Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji kutoka pato la taifa ni hatua ya kwanza tu katika kufanikisha SDGs Afrika-UNCTAD

 Katibu Mkuu wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi
UNCTAD
Katibu Mkuu wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi

Uwekezaji kutoka pato la taifa ni hatua ya kwanza tu katika kufanikisha SDGs Afrika-UNCTAD

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Wakati dunia imeanza muongo wa mwisho kuelekea ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa au SDGs, mwelekeo wa mataifa katika kufanikisha malengo hayo unaathiriwa na mambo mbali mbali ikiwemo migogoro ya kimataifa.

Awali akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Mukhisa Kituyi, Katibu Mtendaji wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa amelinganisha hali ilivyo sasa baada ya mkutano wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo endelevu wa Addis Ababa mwaka 2015 na mwaka jana baada ya mkutano wa New York wa ufadhili.

(Sauti ya Dkt. Kituyi)

"Tangu ule mkutano wa Addis Ababa Julai mwaka 2015, mazingira ya kimataifa ya kuchangia maendeleo yamedidimia. Kwanza kabisa, majadiliano kuhusu biashara yamewacha mambo ya maendeleo yanaongea mambo ya geo-poliitics, siasa kati ya Uchina na Marekani. Pili, teknolojia tulidhania itatuchangia pakubwa kuendeleza lengo la mwaka 2030 lakini ukweli ni kwamba teknolojia sasa imekuwa matego ya kwa siasa ya mvurugano kati ya Marekani na Uchina. Kwa mataifa mengi, ile ahadi tulipata kwamba wawekezaji watalenga uwekezaji katika mitaji ya kuendeleza agenda ya 2030, wengi sana hawaonekani ni kama wanaendelea, mitaji inadidimia, inapunguka kimataifa. Wengi wanawekeza mataifa ya Asia, mataifa ya Afrika kweli hata ile mitaji tunapata sasa imepunguka kuliko ile ilikuwa wakati tulipotoa hizo ahadi. Sasa changamoto kubwa ni kuona ni mbinu gani tutatumia sasa hivi ili kujaribu kutekeleza yale tulikuwa tunatarajia. Mbinu ya kuwekea uzito ni uwekezaji kutoka nyumbani, sio sana uwekezaji wa Umma katika mataifa ya kiafrika utakuwa na maana sana. Pili, kutafuta mbinu za kupunguza uporaji wa mali ya umma hususan kampuni kuu za kimataifa kukwepa kulipa kodi katika mataifa ya kiafrika. Tatu, ni kuutumia teknolojia endelevu kupunguza mizigo na kueneza kuepo fursa kwa watu hususan wanaoishi katika sehemu ambazo zina changamoto kufika masoko ya kimataifa".

Na kuhusu uwezekano wa nchi za Afrika kutimiza malengo hayo kwa kutumia pato la taifa bila kutegemea uwekezaji kutoka nje amesema

(Sauti ya Dkt. Kituyi)

"Kweli mapato ya kitaifa ndiyo hatua ya kwanza na ya maana sana kutekeleza maendeleo tunayotarajia pekee yake haitoshi. kwa mfano, uwekezaji katika mbinu za kupunguza madhara katika mazingira kulingana na mataifa hio bei haiwezekani kutolewa kwa mataifa yanayoendelea. Na wale wanaochangia pakubwa  shida ya kimataifa , ni mataifa ambayo yameendelea. lakini wengi wao sasa unaona wanaaza kuwa na shida ya kukana mabadiliko ya tabianchi, wanajifanya kana kwamba ulimwengu hauna shida ya mabadiliko ya tabianchi. Hiyo ni sehemu moja, lakini ya pili, nikweli kwamba mataifa yenyewe yanaweza kulainisha mipangilio yao ili kuboresha zaidi mazingira  ya wananchi kuwekeza na kujimudu ndio lengo kubwa la maana. Pili, kufungua soko ya Afrika  kunachangia pakubwa kufungua fursa mpya za biashara. Kati ya mataifa ya kiafrika, angalau inaweza kupunguza ile gharama ya  kutokuwa na fursa nyingi katika soko za kimataifa". 

Na akijibu namna UNCTAD inavyozisaidia nchi za kiafrika kuweza kutambua  kuwa mambo yote hayo yanaingiliana ukiwekeza mahali pamoja pekee yake lazima kuna kwingine amesema  

"Kuna mradi ambao umekuwa wa maana sana kwetu kama diagnostic studies tunafanya utafiti kubainisha kila taifa limefikia kiwango gani  katika kuunda miundo misingi ya kidijitali , limefika kiwango kigani kueneza somo katika vyuo vikuu katika mtaala wa shule hususan vyuo vikuu inalengana na mahitaji ya soko ya kidijitali , wamewekeza nadhani katika sheria za kuzuia walaghai wasipore kutoka kwa wananchi ambao hawafahamu kuna sheria ambazo zinasaidia malipo ya elektroniki. Sasa haya yote yanasaidia mataifa kujua kusema sasa unaweza kutafuta wawekezaji waweze wakusaidie kuboresha mazingira ili iwe fursa ya kitaifa. La pili, tunafanya utafiti kumataifa, sema mielekeo iko namna gani katika nchi ambazo zimepata miundo msingi ya kidijitali. Ni vitu vigani vinafanywa vibaya kwa mfano ni mbinu gani tunaweza kutumia kama kampuni kubwa kama google na facebook na shopforce wanapata ujumbe kuhusu watu kwa bure. Wao wanakuuliza tu, nina umri fulani ninakipenda chakula fulani  nina watoto wangapi matarajio yangu , nawanatumia hii kuuza kupata faida yao. Sasa hio faida ni yao pekee yao? Au inapaswa igawanywe na waliowapatia huo ujumbe. Sasa hayo ni mambo ambayo tunaleta katika mjadala katika mambo ya kimaendeleo kwamba faida kubwa ambayo inatolewa katika mataifa yetu ingine inastahili kuwa kama kodi kwetu".

Alimalizia kwa kueleza jinsi serikali zinavyopokea ushauri wao 

"Changamoto kubwa ilikuwa kwamba zile zilizokuwa zinawachwa nyuma hazikuwa zinaona faida ya kujiwezesha. Lakini serikali zote sasa zinaona kwamba zinapoteza fursa, zinaanza kuharakisha mienendo yao pia wanaanza kutuuliza tuwasaidie kupiga hatua kama wengine wanavyopiga".