Mukhisa Kituyi atangaza kujiuzulu Februari 15, Katibu Mkuu amshukuru kwa mchango wake
Katibu Mkuu wa kamati ya Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi amemwelezea Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu nia yake ya kujiuzulu kutoka nafasi hiyo kuanzia tarehe 15 mwezi ujao wa Februari.