Mzigo wa madeni ni sumu kwa maendeleo endelevu-Kituyi
Mzigo wa madeni ni sumu kwa maendeleo endelevu-Kituyi
Kuendelea kuwepo kwa madeni hususan kwa mataifa yanayoendelea barani Afrika ni moja ya changamoto ambayo inakwamisha maendeleo katikabara hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu Mtendaji wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa mkutano wa uchangisahji fedha kwa ajili ya maendeleo endelevu mapema mwezi huu, amesema mzigo huo mkubwa wa madeni unakwamisha nchi kupiga hatua ya kusongesha mbele miradi ya maendeleo ambayo itazisaidia nchi katika utekelezaji wa ajenda ya kimataifa ya 2030 akisema
(Sauti ya Kituyi)
“Mataifa talriban 11 yana changamoto ya madeni amabayo yalikopeshwa na mataifa na mashirika binafsi ya Ulaya, madeni hayoyanapunguza sana uwezo wa serikali kuweza kuwekeza katika maendeleo endelevu pia katika kuimarsiha stadi zinazohitajika kuimarisha mataifa hayo.”
Kwa mantiki hiyo amesema wajibu wa mashirika kama UNCTAD ni
(Sauti ya Kituyi)
“Wajibu wetu ni kutambua mbinu zinazoweza kupunguza gharama na mzigo wa madeni kama njia moja ya kunusura mataifa ambayo ayankabiliwa na changamoto kutokana na uwepo wa madeni, pia kutathmini mbinu ambazo zimetumiwa na mataifa mengine na kufaulu katika kutatua changamoto ya madeni kuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa yaliyo na madeni.”