COVID-19 bado ni dharura ya afya ya umma duniani- WHO
Ugonjwa wa COVID-19 bado ni tishio la afya ya umma duniani na kwa mantiki hiyo dharura itokanayo na janga hilo iliyotangazwa miaka mitatu iliyopita itaendelea, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus.