Baraza Kuu laidhinisha bajeti ya UN kwa 2020 ni zaidi ya dola bilioni 3

28 Disemba 2019

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Ijumaa jioni limeidhinisha bajeti ya Umoja huo kwa mwaka 2020 ambayo ni jumla ya dola 3,073,830,500. 

Bajeti hii ni ongezeko la dola takribani milioni 8 zaidi ya fedha iliyoombwa awali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Hatua hii ni ya kwanza tangu mwaka 1973 ambapo Umoja wa Mataifa unaidhinisha bajeti ya mwaka mmoja tu badala ya miaka miwili. 

Kamati ya tano ya Baraza Kuu ambayo ndio husimamia masuala ya uongozi na bajeti ya Umoja wa Mataifa ndio iliyopitisha bajeti hiyo mapema Ijumaa na baadaye ndipo Baraza Kuu likaitathimini na kuiidhinisha kutokana na ripoti za kamati mbalimbali za Baraza Kuu.

Heko Baraza Kuu kwa kazi nzuri

Katika kuzipongeza kamati mbalimbali kwa kazi nzuri na mafanikio ya kuhitimisha kazi zao, Rais wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande amesema maamuzi waliyofanya ni ufunguo wa utendaji bora wa Umoja wa Mataifa na kuongeza kwamba, “mapendezo ya mipango ya bajeti yam waka 2020 ambayo inatoa rasilimali muhimu kwa sekretariati ya Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yake mbalimbali , pia inatuandaa kwa kuingia muuongo wa hatua kwa ajili ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs.”

Kuanzia mwakani 2020 nchi zitaanza kuongeza juhudi zake kuelekea utimizaji wa SDGs malengo ambayo nia yake ni kuwa na dunia bora kwa wote huku pia ikilinda mazingira.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter