Hatimaye mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefunga rasmi pazia lake hii leo na kuashiria kuanza kwa mkutano wa 75 wa Baraza hilo, ambalo ni moja vyombo vikuu vya Umoja wa Mataifa wenye wanachama 193.
Kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin William Mkapa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hayati Mkapa alikuwa mwanadiplomasia mbobevu na mpigania amani anayeheshimika ambaye alihamasisha maridhiano.
Volkan Bozkir kutoka Uturuki amechaguliwa kuwa Rais wa mkutano ujao wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kufuatia upigaji kura wa aina yake uliofanyika katika mazingira ya sasa ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 yanayozuia kuchangamana.
Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kumeanza mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mabunge duniani, IPU ambapo suala kuu linalomulikwa ni elimu.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Tijjani Muhammad-Bande ambaye alichaguliwa kuchukua wadhifa huo mnamo mwezi Septemba mwaka jana 2019, hii leo jumatatu, awewasilisha kwa nchi wanachama, vipaumbele vyake vya mwaka 2020.
Lugha za asili bado ni muhimu kwa mustakabali wa ulimwengu hivyo tufanye kila namna kuzitunza, ni moja ya kauli alizozitoa rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tijjani Muhammad Bande katika mkutano wa ngazi za juu wa kuhitimisha mwaka wa kimataifa wa lugha za asili uliofanyika hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.
Akitoa taarifa ya kufunga mjadala Mkuu wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York hii leo Rais wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande amesema ushirikiano wa kimataifa unasalia kuwa nguzo muhimu inayokubalika na kutegemewa katika kutatua changamoto za kimataifa miongoni mwa nchi wanachama.