Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa ngazi za juu wa ”Afrika tuitakayo” wafanyika Makao Makuu ya UN

Wasichana na wavulana kutoka kituo cha vijana mjini Nairobi, Kenya wakielezea fikra kuhusu mustakhbali wao kupitia Facebook wakati UNFPA ilipotembelea eneo lao. Na njia hii inasaidia kufanikisha SDGs.
UNFPA/Roar Bakke (maktaba)
Wasichana na wavulana kutoka kituo cha vijana mjini Nairobi, Kenya wakielezea fikra kuhusu mustakhbali wao kupitia Facebook wakati UNFPA ilipotembelea eneo lao. Na njia hii inasaidia kufanikisha SDGs.

Mkutano wa ngazi za juu wa ”Afrika tuitakayo” wafanyika Makao Makuu ya UN

Masuala ya UM

Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kumefanyika mkutano wa ngazi za juu maalum kuangazia masuala ya maendeleo barani Afrika. 

Akizungumza na waandishi kando ya mkutano huo msemaji wa Rais wa Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa- GA Paulina Kubiak amesema mkutano huo ni mpango wa pamoja wa Rais wa GA Abdulla Shahid na Rais wa Baraza la Uchumi na Kijamii la Umojawa – ECOSOC Collen Vixen Kelapile kwa msaada wa Umoja wa Afrika. 

Tweet URL

Mkutano huo uliopewa jina la “Afrika Tuitakayo: Kuthibitisha upya maendeleo ya Afrika kama kipaumbele cha mifumo ya Umoja wa Mataifa” umelenga kufanya tathmini ya maendelo ya utekelezaji wa ajenda ya Maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030- SDG pamoja na ajenda ya Umoja wa Afrika 2063 pamoja na ahadi za kumuiya ya kimataifa kuelekea maendeleo ya Afrika. 

“Katika hotuba yake ya ufunguzi, Rais Shahid alisema kwamba wakati nchi za Kiafrika zinakabiliwa na changamoto zinazofanana na sehemu kubwa ya dunia kuhusiana na vikwazo vya kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi, janga linaloendelea la COVID-19, bei ya mafuta na ukosefu wa usawa, mara nyingi matatizo haya yanazidishwa na udhaifu wa kimsingi ambao unaongeza athari kwenye utekelezaji wa malengo ya SDG.” Amesema Kubiak

Baada ya mazungumzo hayo inatarajiwa kutolewa kwa ‘Wito wa Kuchukuliwa Hatua’ ili kuharakisha kufikiwa maendeleo endelevu ya Afrika, wito ambao unatarajiwa kutolewa na marais wote wawili. takaotolewa na Marais Shahid na Kelapile.

Wanasema kuwa njia bora zaidi ya kushughulikia changamoto za maendeleo ya Afrika ni kwa nchi za Afrika, kwa msaada wa mfumo wa Umoja wa Mataifa, taasisi za fedha za kimataifa na kikanda na wengine, kuongoza juhudi za pamoja.

Mbali na Marais Shahid na Kelapile mwingine aliyezungumza katika mkutano huo wa ngazi za juu ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed.

Tukio hilo linajumuisha majadiliano katika makundi mawili tofauti moja wapo ikiwa ni kukamilisha maandalizi ya mkutano wa COP27 nchini Misri Desemba 2022 huku mwinginee ukiwa ni kuhusu uhamasishaji wa rasilimali za ndani, ufadhili wa kibunifu na ushirikiano wa kimataifa.