Ukifurushwa kwenu mara tano waweza kata tamaa lakini si mimi:Mkimbizi Mustafa

26 Disemba 2019

 Kutana na mkimbizi kutoka Syria Mustafa ambaye hii ni mara ya tano amelazimimika kufungasha virago yeye na familia yake ili kunusuru maisha yake. Pamoja n ayote hayo hakati tamaa ya kurejea nyumbani.

Mustafa mwenye umri wa miaka 36 ambaye yuko ukimbizini katika jimbo la Kurdistan nchini Iraq amejaribu kurejea nyumbani mara kadhaa na kujikuta akilazimika kukimbia tena, tangu kuzuka kwa vira Syria 2011.

(SAUTI YA MUSTAFA)

Hatuwezi kuvumilia hali hii, imekuwa ikiendelea kwa miaka 9 sasa, hatuwezi kuwa na nyumbani tena, tumepoteza nyumba yetu, samani zetu, biashara zetu, ardhi yetu , gari letu, ni hali ngumu sana.”

Mustafa ambaye anakuwa mkimbizi Iraq kwa mara ya tano sasa anasema safari hii hali ni mbaya zaidi lakini hajakata tamaa

(SAUTI YA MUSTAFA)

“Natafuta manailoni na mabomba ya plastiki hapa na pale na nimekopa pesa na kuweza kufungua duka , licha ya kwamba faida ni ndogo sana lakini naweza kuishi”

Pamoja na madhila yote aliyopitia Mustafa bado hajakata tamaa ana ndoto ya kurejea nyumbani Syria, anatumai mara hiyo atakapovuka mpaka itakuwa ni mara ya mwisho anafunga virago.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter