Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzazi wa mpango ni haki ya binadamu: UNFPA

Mtoa huduma azungumza kuhusu afya ya uzazi na wanaume na wanawake. (Picha ya maktaba)
Diana Nambatya/Photoshare
Mtoa huduma azungumza kuhusu afya ya uzazi na wanaume na wanawake. (Picha ya maktaba)

Uzazi wa mpango ni haki ya binadamu: UNFPA

Afya

Uzazi wa mpango sio tu ni suala la haki za binadamu bali pia ni kitovu cha uwezeshaji wa wanawake, kupunguza umasikini na kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s

Kauli hiyo imetolewa na Dr. Natalia Kanem mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu  duniani , UNFPA, katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani ambayo hufanyika kila mwaka Juali 11 safari hii ikibeba kauli mbiu “afya ya uzazi ni haki ya binadamu”

Dr. Kanem amekumbusha kuwa miaka 50 iliyopita dunia itangaza kwamba wazazi wana haki za msingi za binadamu za kuamua kwa wajibu na kwa uhuru idadi ya watoto wanaotaka kuzaa na wapishane kwa umri gani.

Amesema tangu azimio hilo lililotangazwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa  mjini Tehran 13 Mai 1968, bado katika nchi zinazoendelea takriban wanawake milioni 214 wanakosa huduma ya njia salama na zinazofaa za uzazi wa mpango kwa sababu mbalimbali, kuanzia ukosefu wa taarifa au huduma hadi kutopata msaada kutoka kwa wenzi wao au jamii.

Samwel Msokwa ni afisa mwandamizi wa UNFPA Tanzania anayehusika na idadi ya watu na maendeleo , anasema taifa hilo limepiga hatua

(SAMWELI MSOKWA CUT 1)

Licha ya mafanikio bado kuna changamoto na ndio wanazozipigia chepuo kwa sasa

(SAMUEL MSOKWA CUT 2)

UNFPA
Family planning at 50

 

Kwa mujibu wa UNFPA hali hii inatishia uwezo wa wanawake hao kujijengea mustakhbali bora kwa ajili yao, familia zao na jamii zao. Shirika hilo linasaidia juhudi za uzazi wa mpango katika nchi zinazoendelea kwa kuhakikisha upatikanaji wa njia za kisasa na dawa , kuimarisha mifumo ya afya ya kitaifa na kwa kuchagiza usawa wa kijinsia ili kufikia malengo hapo 2030, lakini linasema haliwezi kutimiza yote hayo pekee yake ,hivyo  katika siku hii ya idadi ya watu linatoa wito kwa serikali kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha kuna haki na huduma ya afya ya uzazi kwa wote , ikijumuisha taarifa na huduma za uzazi wa mpango kwa kuzingatia makubaliano ya 1994 kwenye mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo na pia agenda ya maendeleo ya 2030.

UNFPA inasisizita kuwa uwekezaji katika uzazi wa mpango leo ni hazina ya afya na siha njema kwa mamilioni ya wanawake, kwa vizazi vijavyo.