Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viatu ni sehemu ya kumchagiza mtoto kwenda shule-Kidjo 

Angelique Kidjo ambaye ndiye muasisi wa wakifu wa Batonga akitoa maelfu ya viatu kwa wasichana nchini Benini.
UN News
Angelique Kidjo ambaye ndiye muasisi wa wakifu wa Batonga akitoa maelfu ya viatu kwa wasichana nchini Benini.

Viatu ni sehemu ya kumchagiza mtoto kwenda shule-Kidjo 

Msaada wa Kibinadamu

Nchini Benin zaidi ya watoto wa kike 67,000 wa umri wa kati ya miaka 6 na 17 wiki hii wamepokea zawadi ya viatu kama sehemu ya ushirikiano baina ya wakfu wa Batonga unaosimamiwa na mwanamuziki nyota Anjelique Kidjo, shirika la TOMS na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. 

Katika eneo la Batonga nchini Benin balozi mwema wa UNICEF msanii Angelique Kidjo ambaye ndiye muasisi wa wakifu wa Batonga akiwasili na kulakiwa na wenyeji wake wanaompeleka moja kwa moja kwenye shule ya wasichana ya Parakou Mathieu Bouke kukutana na wanafunzi wasicha  waliompokea kwa shangwe na kuimba moja ya vibao vyake maarufu

Kikubwa kilichompeleka ni kuwagawia wasicha hao zaidi ya 300 viatu na kutoa ujumbe muhimu akisema viatu ni sehemu ya fahari wanayoihisi wale wanaotembea wamevivaa na kwamba

 (SAUTI YA ANGELIQUE KIDJO)

Wasichana wanatembea mwendo mrefu kwenda shuleni. Na wasichana wengi waliopelekwa shule wanakosa kuhudhuria shule kwa sababu kuna kitu kilichowachoma au kuwaumiza mguuni na wakapata madhara.”

Bi. Kidjo meongeza kuwa

(SAUTI YA ANGELIQUE KIDJO )

“Kama huna viatu na unatakiwa kutembea mwendo mrefu pekupeku utawezaje kuamka asubuhi na kusema nataka kwenda shule? Hivyo viatu ni sehemu ya kujiamini, na ni suala la uwezeshaji, na hicho ndicho tukifanyacho UNICEF na wakifu wa Batonga.”

Pamoja na hatua kubwa zilizopigwa katika siku za karibuni, balozi huyo mwema anasema bado kuna kibarua kikubwa cha kufanya ili kumuingiza kila mtoto shuleni asome.

Wasichana Benin wako katika hatari kubwa ya kuacha shule hasa wakati wa kuvuka kutoka shule za msingi kuingia sekondari, na takwimu zinaonyesha wasicha 2 kati ya 3 wanakosa elimu ya sekondari nchini humo, huku umasikini ukiwa moja ya sababu kubwa kwa wasicha kukosa elimu na asilimia 43 ya wasichana kutoka kaya masikini hawajawahi kutia mguu darasani.

Zawadi hiyo ya viatu imewalenga wasichana kutoka majimbo ya Alibori, Borgou na Zou nchini Benin.