Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante MINUSCA kwa kuwa kimbilio letu- Mkimbizi Birao

Walinda amani wa MINUSCA wakiwa doriani mjini Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.
MINUSCA
Walinda amani wa MINUSCA wakiwa doriani mjini Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Asante MINUSCA kwa kuwa kimbilio letu- Mkimbizi Birao

Wahamiaji na Wakimbizi

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSCA, umechukua hatua kuimarisha ulinzi kwa wakimbizi wa ndani waliofurushwa makwao kufuatia mapigano ya mwezi uliopita. 

Eneo la Birao, nchini Jamhuri ya Afrika Kati, CAR, wakimbizi wa ndani, wanawake, wanaume na watoto wakiwa kwenye kituo cha kijeshi cha MINUSCA, ikiwa ni kimbilio lao baada ya mapigano ya mwezi uliopita kati ya makundi mawili yaliyojihami ya FPRC na MLCJ.

Shughuli za kawaida zinaendelea kwenye makazi haya karibu na Uwanja wa ndege ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Zambia wameimarisha doria kulinda raia  hawa ikiwa ni sehemu ya jukumu lao.

Luteni Kanali Teddy Tembo ni kamanda wa kikosi cha Zambia mjini Birao na anasema, "tuna takribani wakimbizi wa ndani 14,000 karibu na kambi yetu. Si kazi rahisi. Tunaweka vituo vya ukaguzi kuhakikisha wababe hawaingii Birao.”

Kitendo cha kupata hifadhi kimeleta nafuu kwa wakimbizi wa ndani kama asemavyo mkimbizi Zacharia  Adam ambaye anasema kwamba, “hapa kuna usalama. Kama tusingalikuwa salama hapa, usingalimuona mtu yeyote.”

Tayari mamlaka za eneo hili zinaendesha kampeni kuhakikisha hakuna silaha zinaingizwa kwenye kituo hiki cha kuhifadhi huku shirika la kiraia la ODESCA likisema kuwa kwa saas kituo kicho kiko salama na hakuna changamoto nyingi.

Pamoja na usalama, MINUSCA inawasaidia kuimarisha huduma za usafi na kujisafi kwenye kituo hiki ambacho wengi wamesaka hifadhi.