Tunashukuru uwepo wa UN  kwenye makazi yetu- Imam CAR

24 Oktoba 2019

Ikiwa leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ambao moja ya jukumu lake la kuanzishwa miaka 74 iliyopita lilikuwa ni kusongesha amani, tunaangazia jinsi kupelekwa kwa polisi wa Umoja wa Mataifa kwenye kambi  ya wakimbizi wa ndani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Ndege iliyomchukua Mkuu  wa polisi kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, Meja Jenerali Pascal Champion ikitua katika uwanja wa ndege wa Birao, Kaskazini- Mashariki mwa taifa hilo ambako ghasia za mapema mwezi uliopita zilifurumusha maelfu ya raia.

Lengo la ziara hii sasa ni kukagua doria za pamoja kati ya vikosi vya serikali na  Umoja wa Mataifa zinazofanywa kwenye vituo vya ulinzi wa raia ambapo Meja Jenerali Pascal Champion anasema doria hizo za pamoja ni njia bora zaidi za kusaidia raia.

Vikosi vya usalama vya taifa vilifika eneo hilo tarehe 24 mwezi uliopita ambapo mkuu huyu wa polisi MINUSCA baada ya  ukaguzi anasema..

"Kwa kuwasili kwa polisi na askari  hawa hapa Birao, tunaweza kuboresha vitu vingi sana, si kila kitu lakini tunaweza kufanya hali kuwa bora zaidi.”

Raia nao hawakuficha hisia zao kama asemavyo Mustapha Younous, Imam wa msikiti mkuu wa Birao.

"Tuna furaha sana kwa uwepo wa polisi na askari hawa ambao wamewasili hapa.”

Ulinzi wa raia unaenda sambamba na kuzuia silaha kuingia kambini na hivyo Kamishna wa Polisi mjini Birao anasema kuwa watu hawapaswi kuingia na visu.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud