Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSCA na wakazi wa Birao CAR washirikiana kujenga makazi mapya ya raia

Walinda amani kutoka Zambia wakisafisha mji wa Birao pamoja na wenyeji.
UN/MINUSCA - Hervé Serefio
Walinda amani kutoka Zambia wakisafisha mji wa Birao pamoja na wenyeji.

MINUSCA na wakazi wa Birao CAR washirikiana kujenga makazi mapya ya raia

Amani na Usalama

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ushirikiano kati ya  ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSCA pamoja na raia waliofurushwa makwao kufuatia mapigano ya mwezi Septemba kwenye eneo la Birao nchini humo uwemewezesha wakimbizi hao sasa kupata makazi ya muda yaliyo salama.

Wananchi hawa kutoka eneo la Birao nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ambao walifurushwa makwao kutokana na mapigano na wakasaka hifadhi kwenye uwanja wa  ndege karibu na kambi ya MINUSCA.

Nats..

Hapa wanapatiwa maelezo na Bessan Vikou, Mkuu wa ofisi ya ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa, MINUSCA, mjini Birao wakati huu ambapo pande mbili hizi zinashirkiana kuandaa makazi salama zaidi ya wakimbizi hawa wa ndani.

(Sauti ya Bessan Vikou-)

“Hapa tunalazimika kuanzisha kijiji kidogo. Kijiji hiki kitafanya wakimbizi hawa, ambao wana hofu, na ambao nyumba zao zimetiwa moto na maduka yao kuporwa , waweze kulala wakati wakisubiri mashauriano ya kusaka suluhu. Kwa sasa, ni msimu wa mvua, na hali ya kwenye kambi si nzuri.”

Wakati kambini ulinzi unaendelea, kwenye eneo jipya la makazi, usafishaji wa eneo hilo unaendelea..na mmoja Rais wa chama cha wanawake wa CAR mjini Birao, Fatima Ahamat anasema..

Nats…

(Sauti ya Fatima Ahamat)

"Pale kuna magonjwa mengi sana. Iwapo nitaishi pale nitaweza kufariki dunia. Hapa kwa upande mwingine ni pasafi. Nitahamia hapa.”

Ama hakika umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na hili limedhihirishwa na ushirikiano kati ya MINUSCA na raia huko Birao.