Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu amuhakikishia rais wa DRC msaada wa kupambana na Ebola

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alipokutana na rais wa DRC  Félix Antoine Tshilombo.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alipokutana na rais wa DRC Félix Antoine Tshilombo.

Katibu Mkuu amuhakikishia rais wa DRC msaada wa kupambana na Ebola

Afya

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, leo amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano wa ngazi ya Baraza Kuu la Umoja huo unaoendelea jijini New York Marekani.

Katika mazungumzo yao Rais Felix Tshisekedi Tshilombo na Antonio Guterres wamejadili masuala mbalimbali  yanayotia wasiwasi ikiwemo yale ambayo waliyajadili wakati Katibu Mkuu alipozuru DRC mwezi Septemba mwaka huu.

Miongoni mwa masuala hayo ni hali ua usalama na mlipuko wa Ebola unaoendelea kutoa changamoto kubwa nchini DRC hususan katika eneo la Mashariki .

Mbali ya Ebola wawili hao alijadili pia changamoto zingine za kibinadamu pamoja na masuala ya wakimbizi, kipindupindu na msaada wa Ebola ambao Katibu mkuu amemuhakikishia Rais Tshisekedi Tshilombo kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa kwa nchi hiyo.