Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlo wa asili Mediterranea ni muhimu kwa SDGs:FAO

Hulka na utamaduni wa kuhifadhi vyakula vya asili ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Hulka na utamaduni wa kuhifadhi vyakula vya asili ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Mlo wa asili Mediterranea ni muhimu kwa SDGs:FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kwa kushirikiana na serikali ya Italia wanapigia chepuo umuhimu wa mlo wa Mediterania. 

Katika taarifa yao iliyotolewa leo wadau hao wamesema hulka na utamaduni wa kuhifadhi vyakula vya asili ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Wameongeza kuwa fursa kwa wote kuweza kupata lishe bora kama mlo wa Mediteranea ni kichocheo ya kutimiza ajenda ya mwaka 2030 na mlo huo unapaswa kuchagizwa na kulindwa.

Ujumbe huo umetolewa kwenye tukio maalum la leo lililoandaliwa na FAO na serikali ya Italia kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu mlo wa Mediterranea na kuelimisha ni jinsi gani unaweza kusaidia kufikia SDGs.

Tukio hilo ambalo ni la kwanza katika mfululizo wa matukio yatakayojikita na masuala ya mlo wa Mediterranea limejikita zaidi katika asili, historia, utamaduni nna muundo wa mlo wa Mediterranea na pia misingi inayoambatana na mlo huo.

Tukio hilo limewaleta pamoja wataalam wa mlo wa Mediterranea kuanzia wataalam wa masuala ya chakula na viumbe, wataalam wa lishe, wawakilishi wa serikali ya Italia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wanazuoni ambao wamesisitiza kwamba kuendeleza utamaduni, vyakula vya asili na uzalishaji wa vyakula hivyo  vitazisaidia nchi nyingi kupiga hatua katika utekelezaji wa SDGs.

Faida za mlo wa Mediterranea kwa SDGs

Mlo wa mediterránea unachagiza uzalishaji wa vyakula kwa asili na mfumo wa matumizi yake. Pia unapigia chepuo mfumo wa matumizi ya mlo huo, kilimo endelevu, kulinda mazingira na una kiasi kidogo sana cha uchafuzi wa mazingira amesema mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu kwenye tukio hilo lililofanyika kwenye makao makuu ya FAO mjini Roma.

Mkuu huyo wa FAO pia ameonya kwamba “mlo wa Mediterranea kama ilivyo mingi ya asili kote duniani inaanza kutoweka kutokana na watu kukumbatia hulka za za kisasa za ulaji, wakitegenea saisi mlo rahisi kutengeneza chaguo linalotolewa na maduka mengi ya chakula na wauzaji wa vykula vilivyoandaliwa kwa muda mrefu na kuhifadhiwa.”

Ameongeza kuwa sababu kubwa ya hulka ya watu kubadilika ni pamoja na ongezeko la idadi ya watu, utandawazi, ukuaji wa mija na shinikizo katika uchumi ambazo zote zinaathiri mfumo wetu wa chakula , mlo na mfumo wa matumizi . Hata yanachangia kula milo isiyo na lishe bora kwa afya za watu na kuleta madhara makubwa  kwa afya, maisha ya watu na uchumi w anchi husika.