Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvuvi haramu na usiofuta kanuni ni sumu ya maendeleo na mazingira:FAO

Wavuvi kutoka Kenya wakiwa katika harakati za uvuvi kwenye ziwa Victoria ambako Sangara ndiko makazi yake zaidi
FAO/Ami Vitale
Wavuvi kutoka Kenya wakiwa katika harakati za uvuvi kwenye ziwa Victoria ambako Sangara ndiko makazi yake zaidi

Uvuvi haramu na usiofuta kanuni ni sumu ya maendeleo na mazingira:FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na uvuvi haramu na usiofuata kanuni (IUU) shirika la chakula na kilimo FAO limezitaka nchi kote duniani kuchua hatua kufuata nyayo za Thailand ili kukabiliana na tatizo hilo linaloelekea kumea mizizi. 

Shirika la FAO linasema Thailand ambayo ni msafirishaji wa tatu mkubwa wa samaki duniani hivi sasa imeongeza juhudi za kupambana na uvuvi haramu ili kufikia lengo la rasilimali endelevu za baharí. Tangu mwaka 2015 Thailand ilitathimini upya sheria na mifumo yake na kisha kuandaa mpango wa kitaifa wa kuchukua hatua dhidi ya uvuvi haramu, usioripotiwa na usiofuata kanuni, IUU.

Miongoni mwa hatua hizo ni kufungua kituo cha ufuatiliaji wa masuala ya uvuvi katika idara ya uvuvi ya serikali ambacho kinahitaji vyombo vyote vya kimataifa vinavyovua kupatiwa leseni na kutumia mfumo maalum unaonasa shughuli zote za uvuvi au (VMS ) na pia kutekeleza programu ya ukaguzi kabla ya kuondoka na vinapowasili bandarini. Simon Nicol ni afisa wa uvuvi wa FAO

SAUTI YA SIMON NICOL

“Kupotea kwa samaki kutokana na uvuvi haramu na usiofuata kanuni  kunaathiri uwezo wetu wa kutambua samaki wetu ni endelevu kiasi gani na kwa kiwango gani tunapaswa kuvua kiwango ambacho kitakuwa kinazingatiwa na sekta zetu za uvuvi. IUU inapokonya pato la wavuvi halali na uchumi ambao ungetegemewa katika sekta hizo za uvuvi.”

Mwezi Januari mwaka huu Muungano wa Ulaya umeindoa Thailand katika orodha ya nchi zilizoshindwa kukabiliana na uvuvoi haramu na usiofuata kanuni baada ya kubaini kwamba imechukua hatua madhubuti kushughulikia sekta yake ya uvuvi ambayo ni ya mabilioni ya dola. Akifafanua baadhi ya mikakati yao Jaruwan Sonphatkaew mkaguzi wa serikali wa sekta ya uvuvi anasema ukaguzi wa kina unafanyika kuanzia kwenye vyombo hadi nyaraka mfano

SAUTI YA JARUWAN SONPHATKAEW

“Tunalinganisha nyaraka asilia na nakala walizowasilishakatika maombi yao, na baada yah apo tunakagua mfumo wa ufuatiliaji wa chombo cha uvuvi , au VMS na kisha tunatoa ripoti ya ukaguzi PIR na baada yah apo ndio tunaruhusu upakuaji wa mzigo au matumizi ya bandari.”

Uvuvi haramu una usiofuata kanuni unakadiriwa kuwa ni tani milioni 26 kwa mwaka au sawa na moja ya tano ya samaki wote wanaovuliwa  kote duniani na mbali ya kupora rasilimali za jamii pia unachangia katika uharibifu wa mazingira ya bahari na kuathiri viumbe. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa idara ya uvuvi ya Thailand Adsorn Promthep soko ndio chachu ya kuendelea kwa uvuvi huo

SAUTI YA ADSORN PTOMTHE

“Soko ndio kitu kimoja ninachodhani ni nyenzo muhimu ya kukomesha au kupambana na uvuvi haramu, sio tu kujaribu kuwakamata wakiutekeleza wanapovua kwani ni vigumu sana kwa sababu bahari ni kubwa , hata hivyo endapo watashindwa kuuza samaki hao hio ndio sehemu muhimu ya ambayo tunaweza kuidhibiti.”

Tarehe 5 Disemba 2017 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliafiki kupitisha azimio lililopendekezwa na FAO kuhusu uvuvi endelevu na kuitangaza Juni 5 kila mwaka kuwa ni siku ya kimataifa ya kupinga uvuvi haram una usiofuata kanuni na maadhimisho ya kwanza yalifanyika mwaka jana 2018.

 

TAGS: Uvuvi haramu, Thailand, FAO, IUU, SDGs