Jukwaa la kimataifa kuhusu usalama wa chakula na biashara likikunja jamvi hii leo huko Geneva, Uswisi, mashirika ya Umoja wa Mataifa yametaka mataifa kuzingatia siyo tu usalama wa chakula kinacholiwa bali pia mchango wake katika afya ya mlaji ili kudhibiti ongezeko la matipwatipwa duniani.