Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyumba za wajawazito ni kiungo muhimu kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua-UNFP Ethiopia

Wanawake wakiwa kwenye kituo cha afya nchini Ethiopia
World Bank/Binyam Teshome
Wanawake wakiwa kwenye kituo cha afya nchini Ethiopia

Nyumba za wajawazito ni kiungo muhimu kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua-UNFP Ethiopia

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFP nchini Ethiopia kwa ushirikiano na serikali wameanzisha nyumba maalum za wajawazito ambapowanasubiria hadi pale wanapojifungua ili kupata huduma katika kituo cha hospitali hizo na kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

 

Play Natts

Hii ni sauti ya Ekram Yassin, akisema amerejea nyumbani baada ya wiki tatu na kwamba familia yake inafurahi amerudi akiwa salama yeye na mtoto wake aliyejifungua.

Idadi ya wanawake kama hao ambao wanakaa katika nyumba za wajawazito katika wiki zao za mwisho za ujauzito inaongezeka huku wakipata huduma muhimu kutoka kwa wataalam.

Wizara ya afya nchini Ethiopia kwa kushirikiana na wadau wanaendesha nyumba hizo katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini. Bettina Maas ni mwakilishi mkazi wa UNFPA nchini Ethiopia

(Sauti ya Bettina)

“Kwa UNFPA kutokomeza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua ni nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, nimeshawishika kwamba nyumba za wajawazito ni muhimu katika kupunugza idadi ya vifo vya wanawake na watoto wakatia wanapojifungua nchini Ethiopia na ndio sababu UNFPA itaendelea kuimarisha msaada wake katika kufanikisha mpango huo.”

Wanawake wakati wakisubiri kujifungua katika nyumba hizo wanapata huduma za afya. Etenesha Abate ni mama mjamzito katika moja ya nyumba hizo

(sauti ya Etenesha)

“Nilikuwa nakuja katika kliniki ya wajawazito katika kituo hiki cha afya na nililazimika kusafiri mwendo wa saa tatu, walinishauri kuishi hapa ili nisihatarishe uja uzito wangu.”

Mpango huu wa nyumbza za wajawazito tayari umezaa matunda kama anavyosema mkunga Tesfaye Yesmaw

(Sauti ya Tesfaye)

“Wanawake wengi wanajifungua hapa huku wakipokea huduma kutoka kwa wataalam, katika kipindi cha miezi mitatu wanawake 31 kutoka mashinani ambako hakuna magari ya kubeba wagonjwa wamekuja hapa kujifungua.”

Ushiriki wa jamii umefnikisha nyumba hizo kwani hao ndio wajenzi wa nyumba hizo na huchangia chakula huku pia wakiwashawaishi wanawake wajawazito kuenda katika nyumba hizo.