Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chaguo la idadi ya watoto bado ni kitendaliwi kwa wengi- UNFPA

Mama na mwanae katika kambi ya wakimbizi wa ndani karibu na kijiji cha Mopti vitongoji vya mji. Uwezo wa mwanamke kuchagua watoto anaotaka bado ni kitendawili-UNFPA
UN Photo/Marco Dormino
Mama na mwanae katika kambi ya wakimbizi wa ndani karibu na kijiji cha Mopti vitongoji vya mji. Uwezo wa mwanamke kuchagua watoto anaotaka bado ni kitendawili-UNFPA

Chaguo la idadi ya watoto bado ni kitendaliwi kwa wengi- UNFPA

Wanawake

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya idadi ya watu imeonyesha bayana uhusiano mkubwa kati  ya idadi ya watoto na na fursa ya mtu kupata haki ya msingi ya huduma za afya ya uzazi.

Ikipatiwa jina la Uwezo wa kuchagua, ikimaanisha mtu awe na fursa ya kuchagua idadi ya watoto anaotaka kuwa nao, iwe ni wengi au wachache ripoti imebaini kuwa haki  ya mtu kupata huduma za afya ya uzazi ina uhusiano mkubwa na haki nyingine kama vile huduma bora za afya, elimu na ajira.

Mathalani ripoti ina simulizi ya Thereza, mkazi wa Brazil mwenye umri wa miaka 87 hivi sasa ambaye baada ya kuolewa akiwa na umri wa miaka 18 hakufahamu iwapo akijamiiana na mwanaume atapata ujauzito.

Ripoti hiyo ya shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA inasema Thereza ingawa alibeba ujauzito mara 22 , ni watoto 15 ambao walizaliwa salama, mimba nyingine 7 ziliharibika kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya ya uzazi.

Akizungumza wakati wa kuzindua ripoti hiyo, Mkurugenzi wa ofisi ya shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA, huko Geneva, Uswisi Monica Ferro amesema..

(Sauti ya Monica Ferro)

“Pale ambapo haki za afya ya uzazi zinazingatiwa watu wanastawi, ambako hazizingatiwi watu hawana uwezo wa kuchanua, na kiwango cha uzazi kinakuwa kikubwa au kidogo.”

Kwa mantiki hiyo amesema ripoti inatoa mapendekezo kutokana na mazingira ya nchi husika akisema..

(SAuti ya Monica Ferro)

“Ili kufanya fursa ya kuchagua kuwa kitu halisi, ripoti inasema nchi zinaweza kupatia kipaumbele huduma ya bora afya ya uzazi kwa wote, ikiwemo mbinu za kisasa za uzazi wa mpango, kutoa elimu sahihi ya mabadiliko ya mwili kwa kuzingatia umri wa mhusika.”

TAGS: UNFPA, SWPR2018, Afya ya uzazi, idadi ya watu