Ardhi ni rasilimali iliyo katika shinikizo kubwa kutoka kwa binadamu na mabadiliko ya tabianchi:IPCC

Picha ya juu ikionesha eneo la kisiwa cha Mayotte
UN World Oceans Day/Gaby Barathieu
Picha ya juu ikionesha eneo la kisiwa cha Mayotte

Ardhi ni rasilimali iliyo katika shinikizo kubwa kutoka kwa binadamu na mabadiliko ya tabianchi:IPCC

Tabianchi na mazingira

Ardhi ni rasilimali muhimu ambayo iko katika shinikizo kubwa kutoka kwa binadamu na mabadiliko ya tabia nchi, lakini pia inaweza kuwa sehemu ya suluhu ya changamoto hizo imesema ripoti ya jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC.

Ripoti hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi imesema wakati huohuo kuhakikisha kiwango cha joto duniani kinasalia chini ya nyuzi joto 2 kipimo cha selsiasi itawezekana tu kwa kupunguza gesi ya viwandani katika sekta zote ikiwemo ardhi na chakula.

Kwa mujibu wa Hoesung Lee mwenyekiti wa IPCC “serikali ziliipa changamoto IPCC kwa mara ya kwanza kuchukua hatua ya kutathimini kwa kina suala zima la ardhi na mfumo wa mabadiliko ya tabianchi. Na  tumefanya hivyo kwa mchango mkubwa kutoka kwa wataalam na serikali zote duniani. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya ripoti za IPCC asilimia kubwa ya waandishi (53%) ni kutoka katika nchi zinazoendelea.”

Ameongeza kuwa ripoti hii “inaonyesha kwamba udhibiti mzuri wa ardhi unaweza kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi  lakini sio suluhisho pekee. Kupunguza kiwango cha gesi ya viwandani katika sekta zote ni muhimu sana ili kuhakikisha kiwango cha joto duniani kinasalia chini ya nyuzi joto chini ya nyuzi joto 2 katika kipimo cha selsiasi kama sio nyuzi joto 1.5C kipimo cha selsiasi.”

Umuhimu wa ardhi

Ripoti hiyo ya IPCC imesisitiza kuwa ardhi ni lazima iendelee kuzalisha ili kuhakikish uhakika wa chakula kwa idadi ya watu inayoendelea kuongezeka na ongezeko la athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi katika uoto wa asili. 

Na hii inamaanisha kwamba kuna ukomoa wa kiwango ambacho ardhi inaweza kuchangia katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi kwa mfano kupitia kilimo cha mazao yanayoleta nishati na upandaji miti.

Pia imesema nishati itokanayo na kilimo inapaswa kudhibitiwa vyema ili kuepuka hatari ya uhakika wa chakula , bayoanuai na mmomonyoko wa ardhi. Kwa mujibu wa IPCC ripota hili litafanikiwa kutegemeana na sera muafaka na mifumo bora ya utawala.

Ardhi na mabadiliko ya tabianchi

IPCC ripoti inasema ardhi ina jukumu muhimu katika mfumo wa mabadiliko ya tabianchi “kilimo, upandaji miti na aina zingine za matumizi ya ardhi yanachangia asilimia 23% ya gesi ya viwandani inayosababishwa na binadamu. Wakati huohuo ardhi inanyonya hewa ukaa sawa na Karibu theluthi moja ya hewa ukaa inayotoka viwandani .”

Ripoti inaonyesha kwamba kuthibi ardhi kikamilifu inaweza kusaidia kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

“Kuchukua hatua mapema kutapunguza gharama na kuepusha harasa kubwa, kuna vutu tayari tunafanya , tunatumia teknolojia na mipango mizuri lakini vinatakiwa kuongezwa zaidi ili vitumike mahali ambako havitumiki kwa sasa” amesema Panmao Zhai, mwenyekiti mwenza wa jopo la IPCC akiongeza kuwa “Kuta uwezekano mkubwa hapa kupitia matumizi endelevu ya ardhi , kupunguza matumizi na utupaji wa chakula, kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji na matumizi ya nyama nyekundu, kukomesha uchomaji misitu, kuzuia uvunaji wa kupindukia wa misitu kwa ajili ya kuni, na kupungua utoaji wa gesi ya viwandani, hivyo vitasaidia kushughulikia matatizo ya ardhi yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.