Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi ni tishio kwa binadamu na afya ya dunia , hatua zahitajika sasa:IPCC Ripoti

Mwanamke akiwa amembeba mwanaye wakati wa mafuriko mjini Jarkata Indonesia
© WMO/Kompas/Hendra A Setyawan
Mwanamke akiwa amembeba mwanaye wakati wa mafuriko mjini Jarkata Indonesia

Mabadiliko ya tabianchi ni tishio kwa binadamu na afya ya dunia , hatua zahitajika sasa:IPCC Ripoti

Tabianchi na mazingira

Ripoti mpya ya jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC iliyotolewa leo imesema kuchukua hatua sasa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kunaweza Kuchukua hatua sasa “Kunaweza kulinda mustakabali wetu  kwani mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na shughuli za binadamu yanasababisha usumbufu wa hatari na ulioenea katika mazingira yetu na kuathiri maisha ya mabilioni ya watu kote ulimwenguni, licha ya juhudi zinazofanyika kupunguza hatari hiyo.”

Wanasayansi wa jopo hilo wamesema katika ripoti kwamba “Watu na mifumo duni ya ikolojia ndiyo ambayo haiwezi kustahimili na kuathirika zaidi. Ripoti hii ni onyo kali kuhusu matokeo ya kutochukua hatua," ameongeza Hoesung Lee, Mwenyekiti wa IPCC
Inaonyesha kuwa mabadiliko ya tabianchi ni tishio kubwa na linaloongezeka kwa ustawi wetu na sayari yenye afya.
“Matendo yetu leo ndio yatakayounda jinsi watu wanavyojenga mnepo na jinsi mazingira yatakavyohimili hatari zinazoongezeka za mabadiliko ya tabianchi.”
Ripoti hii ni onyo kali kuhusu matokeo ya kutochukua hatua,” alisema Hoesung Lee, Mwenyekiti wa Jopo la Serikali za Kiserikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC). Hatua nusunusu sio chaguo tena."
Hii ni ripoti ya pili katika mfululizo wa ripoti tatu kutoka kwa wanasayansi wakuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi na kuzinduliwa kwake kumekuja zaidi ya siku 100 tangu mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi mjini Glasgow, COP26, kukubali kuongeza hatua za kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzijoto 1.5°C na kuepusha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya hali ya hewa.

Moshi kutoka kwenye kinu cha nyuklia Cattenon Ufaransa
Unsplash/Thomas Millot
Moshi kutoka kwenye kinu cha nyuklia Cattenon Ufaransa


Tunakabiliwa na changamoto kubwa

Kwa hakika kutokana na ushahidi uliopo ripoti hii, ambayo inaangazia athari, kukabiliana na hali na mazingira magumu, inafichua jinsi watu, na sayari, wanavyochanganyikiwa na mabadiliko ya tabianchi.
"Karibu nusu ya wanadamu wanaishi katika maeneo ya hatari hivi sasa. Mifumo mingi ya ikolojia iko katika hatua ya kusambaratika. Uchafuzi wa hewa ukaa ambao haujadhibitiwa unalazimisha walio hatarini zaidi ulimwenguni kwenye maandamano ya vyura hadi katika zahma kubwa" amesema.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 

Katika taarifa yake kuhusu uzinduzi wa ripoti hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wachafuzi wakubwa zaidi duniani ndio wenye hatia ya kuchoma nyumba yetu.”
Ameongeza kuwa kwa kukabiliwa na ushahidi huo wa kutisha, ni muhimu kufikia lengo la kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5, na sayansi inaonyesha kwamba itahitaji dunia kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa asilimia 45 ifikapo 2030 na kutozalisha kabisa hewa hiyo chafuzi ifikapo mwaka 2050.
"Lakini kulingana na ahadi za sasa, uzalishaji wa hewa chafu duniani unatarajiwa kuongezeka karibu asilimia 14 katika muongo wa sasa. Hiyo inaashiria janga. Itaharibu nafasi yoyote ya kusalia katika nyuzi joto 1.5.” 
Moja ya ukweli wa msingi wa ripoti hiyo ni kwamba makaa ya mawe na mafuta mengine kisukuku yanauadhibu ubinadamu, Katibu Mkuu ameeleza, akitoa wito kwa serikali zote za G20 kutimiza makubaliano yao ya kuacha kufadhili makaa ya mawe nje ya nchi, na lazima sasa kufanya hivyo kwa dharura nyumbani. na kusambaratisha meli zao za makaa.

Kimbunga Lota kilisababisha uharibifu mkubwa na mafuriko Nicaragua na kuwaacha maelfu bila makazi
© UNICEF/Inti Ocon/AFP-Services
Kimbunga Lota kilisababisha uharibifu mkubwa na mafuriko Nicaragua na kuwaacha maelfu bila makazi

Aidha, amesema kuwa makampuni makubwa ya mafuta na gesi na waandishi wao pia wako kwenye tahadhari. "Huwezi kudai kuwa kijani wakati mipango na miradi yako inadhoofisha lengo la mwaka 2050 la kutozalisha kabisa hewa ukaa na kupuuza upunguzaji mkubwa wa uzalishaji ambao lazima utokee muongo huu. watu wanaona kupitia skrini hii ya moshi."
Badala ya kupunguza kasi ya uchumi wa hewa ukaa wa dunia, sasa ni wakati wa kuharakisha mpito wa nishati kwa siku zijazo na kuingia katika nishati mbadala, almersema Katibu Mkuu na kutangaza nishati ya mafuta kuwa "mwisho uliokufa kwa sayari yetu, kwa wanadamu, na ndio, kwa uchumi," na ametoa wito kwa nchi zilizoendelea, Benki za maendeleo ya kimataifa, wafadhili wa kibinafsi na wengine kuunda miungano ili kusaidia mataifa makubwa yanayoinukia kiuchumi kukomesha matumizi ya makaa ya mawe.

Kuwekeza kukabili mabadiliko ya tabianchi

Matokeo ya pili ya msingi kutoka kwenye ripoti hii ya IPCC ni habari kidogo Njema, uwekezaji katika kazi ya kukabiliana na hali hiyo.
"Kadiri athari za mabadiliko ya tabianchi zinavyozidi kuwa mbaya hivyo  kuongeza uwekezaji itakuwa muhimu kwa maisha ya kizazi hiki na kijacho. Marekebisho na upunguzaji wa utoaji hewa ukaa lazima ufuatwe kwa nguvu na uharaka sawa. 
“Ndiyo maana nimekuwa nikisukuma kufikia asilimia 50 ya fedha zote za hali ya hewa kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo,” Bw. Guterres ameeleza.
Akibainisha kuwa dhamira ya Glasgow juu ya ufadhili wa kukabiliana na hali hiyo ni wazi haitoshi kukabiliana na changamoto zinazokabili mataifa katika mstari wa mbele wa mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi akisema kuwa anasisitiza pia kuondoa vikwazo vinavyozuia nchi za visiwa vidogo na nchi zilizoendelea zaidi kupata fedha. wanahitaji sana kuokoa maisha na riziki ya kila mtu.

Lengo kuu la Kastibu Mkuu ni kutokomeza uzalishaji wa makaa ya mawe
Unsplash/Markus Spiske
Lengo kuu la Kastibu Mkuu ni kutokomeza uzalishaji wa makaa ya mawe


Kuchelewa maana yake ni kifo


"Tunahitaji mifumo mipya ya kustahiki ili kukabiliana na ukweli huu mpya. Kuchelewa kunamaanisha kifo,” amesisitiza Katibu Mkuu.
Amesema kwamba anapata msukumo kutoka kwa wale wote walio mstari wa mbele wa vita vya mabadiliko ya tabianchi wakipigania suluhu, Katibu Mkuu alisema anajua watu kila mahali walikuwa na wasiwasi na hasira.
“Mimi pia. Sasa ni wakati wa kugeuza hasira kuwa vitendo. Kila sehemu ni muhimu. Kila sauti inaweza kuleta mabadiliko. Na kila sekunde inahesabu muhimu.