Skip to main content

Chuja:

Ardhi

UN/ John Kibego

Vijana wa kike wahimizwa kupigania haki za kumiliki ardhi Uganda.

Wiki hii dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani ambapo sehemu mbalimbali wanawake waliitumia kuonesha kero zao na kutiana moyo. Nchini Uganda, wanawake katika wilaya ya Buliisa wameandamana hadi Makao Makuu ya wilaya hiyo kuwasilisha malalamiko yao wakiitaka serikali ishughulikie changamoto yao ya kunyimwa haki ya kumiliki ardhi.

Sauti
3'51"
UNDP Chad/Jean Damascene Hakuzim

Ukitaka kula, kunywa maji au kupumua ni lazima udhibiti kuenea kwa jangwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua za dharura zichukuliwe ili kulinda na kurejesha ardhi iliyomomonyoka sambamba na ongezeko la kuenea kwa jangwa duniani kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.

Bwana Guterres amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kukabiliana na kuenea kwa jangwa hii leo, ambayo inaenda sambamba na maadhimisho  ya miaka 25 tangu kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na kuenea kwa jangwa.

Sauti
1'50"
UN SDGs

Utoaji haki Uganda usiengue maskini

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yameangazia masuala yote muhimu yanayogusa jamii yetu zama za sasa. Mathalani suala la watu kufurushwa kutoka kwenye nyumba zao au hata kufungwa kinyume cha sheria.

Lengo namba 16 limeangazia  masuala ya upatikanaji wa haki kisheria, ujenzi wa amani na uwepo wa  jamii jumuishi. Ni kwa mantiki hiyo John Kibego amefuatilia usakaji wa haki nchini Uganda katika masuala ya ardhi akizungumza na baadhi ya watu walionyimwa haki zao. Ungana naye  katika makalahii.

Sauti
3'32"
UN News

'Hatuhamihami" bali tunahama na tutarejea- Dkt. Laltaika

Mvutano mkubwa huibuka baina ya wakulima na jamii ya watu wa asili hususan ile ya wafugaji. Mvutano huo ni katika masuala ya matumizi ya ardhi ambapo mara nyingi wafugaji hulaumiwa kutumia ardhi kiholela kutokana na kuhama kwao wanaposaka malisho ya mifugo yao. Umoja wa Mataifa unasisitiza masuala ya matumizi bora ya ardhi kama njia ya kulinda tabianchi Je ni kweli wafugaji  huhamahama? Na je kupitia wafugaji hasa wa jamii ya asili ,dunia inaweza kubadili mweleko wa sasa wa uharibifu wa mazingira na tabianchi. Assumpta Massoi amezungumza na Dkt.

Sauti
4'8"