Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Uchafuzi wa hewa kutoka kwa viwanda unasababisha mabadiliko ya tabianchi.

Ni wakati wa kuacha kuikaanga sayari yetu na kutimiza ahadi za mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo:Guterres

© Unsplash/Ella Ivanescu
Uchafuzi wa hewa kutoka kwa viwanda unasababisha mabadiliko ya tabianchi.

Ni wakati wa kuacha kuikaanga sayari yetu na kutimiza ahadi za mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo:Guterres

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameonya kwamba dunia inaelekea pabaya linapokuja suala la mabadiliko ya tabianchi , ni suala la aibu linaloambatana na ahadi hewa ambazo zinamuweka kila mtu kwenye hatari ya zahma kubwa. 

Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo baada ya ripoti ya jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC, Guterres amesema “Mahakama imefikia uamuzi. Na ni laana. Ripoti hii ya Jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi ni orodha ya ahadi zilizovunjika za hali ya hewa. Ni faili la aibu, likiorodhesha ahadi hewa ambazo zinatuweka kwenye njia ya kuelekea ulimwengu tusioweza kuishi.” 

Amesisitiza kwamba “Hali ni bayana miji mikubwa imeghubikwa na maji, kunashuhudiwa mawimbi ya joto ambayo hayajawahi kutokeam vimbunga vya kutisha, uhaba mkubwa wa maji, kutoweka kwa aina milioni ya mimea na wanyama. Hii sio kiini macho au kutia chumvi bali ni kile ambacho sayansi inatuambia kitatokana na sera zetu za sasa za nishati.” 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linawasaidia wakulima wanaoishi katika mazingira magumu katika viunga vya nje kidogo ya mji mkuu wa Syria, Damascus kukabiliana vyema na mabadiliko ya tabianchi kwa kulima mimea ya dungusikakati isiyo
UN Video
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linawasaidia wakulima wanaoishi katika mazingira magumu katika viunga vya nje kidogo ya mji mkuu wa Syria, Damascus kukabiliana vyema na mabadiliko ya tabianchi kwa kulima mimea ya dungusikakati isiyo

Joto linaongezeka duniani 

Katibu mkuu amesema dunia  iko njiani kuelekea ongezeko la joto la zaidi ya mara mbili ya kikomo cha nyuzi joto 1.5 kilichokubaliwa kwenye mkutano wa viongozi mjini Paris. 

Amesema na hii ni sababu ya baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyabiashara wanasema jambo moja lakini wanachofanya ni kingine, kwa kifupi wanadanganya na matokeo yake ni zahma kubwa, hii ni dharura ya mabadiliko ya tabianchi. 

Wanasayansi wa mabadiliko ya tabianchi wanaonya kwamba tayari tuko karibu na maeneo hatarishi ambayo yanaweza kusababisha athari mbaya za hali ya hewa na zisizoweza kutenguliwa. 

Lakini amesema serikali na mashirika yanayozalisha kiasi kikubwa cha hewa ukaa sio tu yanafumbia macho suala hili bali yanaongeza mafuta kwenye moto. 

“Wanaikaanga sayari yetu, kwa ajili ya maslahi yao na uwekezaji wao wa kihistoria kwenye mafuta ya kisukuku, wakati suluhu za bei nafuu, zipo na zinaweza kutoa ajira zinazojali mazingira, usalama wa nishati, na uthabiti zaidi wa bei.” 

Tuliondoka kwenye COP26 mjini Glasgow tukiwa na matumaini ya kutojua, kulingana na ahadi na ahadi mpya. 

Amesema mkutano wa 26 wa mabadiliko ya tabianchi COP26 kwa kiasi ulitoa matumaini kutokana na ahadi mpya lakini tatizo kubwa ni ongezeko la pengo la uzalishaji hewa ukaa ambalo linapuuzwa.

Mifumo ya uzalishaji chakula barani Afrika imevurugwa kwa kiasi kikubwa kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi na hivi karibuni zaidi janga la Corona.
© FAO/Petterik Wiggers
Mifumo ya uzalishaji chakula barani Afrika imevurugwa kwa kiasi kikubwa kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi na hivi karibuni zaidi janga la Corona.

Sayansi iko bayana 

Guterres amesema kama kuna kilicho bayan abasi ni sayansi ambayo inataka kudhibiti kiwango cha choto duniani kusalia nyuzi joto 1.5. “Tunahitaji kupunguza utoaji wa hewa chafuzi duniani kwa asilimia 45 muongo huu. 

Lakini ahadi za sasa za hali ya hewa zinaweza kumaanisha ongezeko la asilimia 14 la uzalishaji. Na wazalishaji wakuu wengi wakuu wa hewa chafuzi hawachukui hatua zinazohitajika kutimiza hata ahadi hizi zisizotosheleza. Kuwekeza katika miundombinu mipya ya uzalishaji mafuta kizukuku ni wazimu wa kimaadili na kiuchumi. Uwekezaji kama huo hivi karibuni utakuwa mali iliyokwama na doa katika mazingira, na uwekezaji.” 

Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri maeneo ya pwani ya Tunisia yanayoathiri wanadamu na viumbe hai vya baharini.
UNDP Tunisia
Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri maeneo ya pwani ya Tunisia yanayoathiri wanadamu na viumbe hai vya baharini.

Lakini si lazima iwe hivyo.

Guterres amesema ripoti ya leo inalenga kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi. 

Inaweka chaguo zinazowezekana, za kifedha katika kila sekta ambazo zinaweza kuweka hai uwezekano wa kuzuia ongezeko la joto duniani usizidi nyuzi joto 1.5. 

“Kwanza kabisa, ni lazima tuongeze mara tatu kasi ya kuhamia kwenye nishati mbadala. Hiyo inamaanisha kuhamisha vitega uchumi na ruzuku kutoka kwenye mafuta kisukuku hadi kwenye nichati mbadala, sasa. Inamaanisha serikali kukomesha ufadhili wa makaa ya mawe, sio tu nje ya nchi, lakini nyumbani pia.

Inamaanisha kulinda misitu na mifumo ya ikolojia kama suluhu zenye nguvu dhidi ya mabadiliko ya tabianchihali. Inamaanisha maendeleo ya haraka katika kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane. Na inamaanisha kutekeleza ahadi zilizotolewa huko Paris na Glasgow.” 

Wanawake na watoto ni waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi
UNVMC/Laura Santamarìa
Wanawake na watoto ni waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi

Viongozi lazima washike usukani 

Guterres amesema kila mmoja ana wajibu wa kutimiza katika hili kwani “Tuna deni kwa vijana, mashirika ya kiraia na jumuiya za watu wa asili kwa kupiga kengele na kuwawajibisha viongozi.” 

Ameongeza kuwa “Ikiwa unaishi katika jiji kubwa, eneo la mashambani, au katika jimbo la kisiwa kidogo,ikiwa unawekeza soko la hisa, ikiwa unajali kuhusu haki, na maisha ya baadaye ya watoto wetu,ninatoa wito kwako dai kwamba nishati mbadala ianzishwe sasa kwa kasi na kwa kiwango kikubwa, omba kukomeshwa nishati ya makaa ya mawe, na omba uwe mwisho wa ruzuku zote za mafuta kisukuku.” 

Amesisitiza kuwa “Ahadi na mipango ya mabadiliko ya tabianchi lazima igeuzwe kuwa ukweli na kwa vitendo, sasa.m Ni wakati wa kuacha kuchoma sayari yetu, na kuanza kuwekeza katika nishati nyingi mbadala zinazotuzunguka.