Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yaipiga jeki Redio ya serikali Torit ilikusambaza ujumbe wa amani

Paneli za sola ambazo zimetegwa tayari kukusanya nishati hiyo endelevu.
Shutterstock
Paneli za sola ambazo zimetegwa tayari kukusanya nishati hiyo endelevu.

UNMISS yaipiga jeki Redio ya serikali Torit ilikusambaza ujumbe wa amani

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekabidhi paneli 46 za kuzalisha nishati ya jua au sola na vifaa vyake kwa kituo cha redio cha Torit, 97.5 FM kinachoendeshwa na serikali ili kukipa uwezo na kuboresha operesheni za matangazo yake ambayo mara nyingi yanakatika kutokana na tatizo la umeme na mafuta ya jenereta.

Huu mradi wa kuleta mabadiliko katika jamii uliozinduliwa na UNMISS mwezi Machi mwaka huu kwa gharama ya dola 50,000 kwa lengo la kuhakikisha ujumbe wa amani unamfikia kila mmoja kwa kutumia mbinu zote ikiwemo Redio za kijamii zinazowafikia waathirika mashinani.

Paneli hizo za Sola zilizowekwa Alhamisi kwenye kituo cha Redio cha Torit UNMISS imesema sasa kitakiwezesha kituo hicho kutangaza kwa saa 12 kwa siku na kufika umbali wa kilometa 100 mjini Torit jambo ambalo litasaidia wananchi wengi kupata taarifa na ujumbe muhimu.

Katika hafla ya makabidhiano ya panel hizo mwakili wa UNMISS Torit Caroline Waudo amewahakikishia wananchi kuendelea kwa msaada wa mpango huo kwa ajili ya kuhakikisha operesheni zake za kuchaguza Amani na ujumbe unamfikia kila mtu na kwamba

(SAUTI YA CAROLINE WAUDO)

“Nina imani kwamba Redio itatumika vizuri kusambaza ujumbe wa amani ambao utachagiza mshikamano kwenye jamii na kuishi kwa amani miongoni mwa jamii, hata hivyo Redio isitumike kuchagiza hotuba za chuki ambazo zitaleta madhara na kuchochea jamii wakati wa utoaji huduma.”

Kituo hicho cha redio kilianzishwa mwaka 2008 na kilikuwa kikirusha matangazo kwa saa tano tu kwa siku kutokana na uhaba wa umeme na mafuta ya jenereta ambayo alikuwa yakisaiudia kuendesha mitambo ya redio hiyo.

Hadi kufikia sasa UNMISS imekamilisha miradi 16 ya kijamii Mashariki mwa jimbo la Equatoria na kuendelea kushirikisha jamii kwa ajili ya kuchagiza amani na miradi ya maendeleo.