Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunatumia kila mbinu kudhibiti mlipuko wa Ebola:Uganda

Mhudumu wa afya akipima joto la mwananchi kwenye eneo la mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Uganda. Wahudumu wa afya kwenye kituo hiki wamekuwa wakichukua vipimo kubaini iwapo wananchi wana Ebola au la. (12 Feb 2019)
UNICEF/Jimmy Adriko
Mhudumu wa afya akipima joto la mwananchi kwenye eneo la mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Uganda. Wahudumu wa afya kwenye kituo hiki wamekuwa wakichukua vipimo kubaini iwapo wananchi wana Ebola au la. (12 Feb 2019)

Tunatumia kila mbinu kudhibiti mlipuko wa Ebola:Uganda

Afya

Serilikali ya Uganda kupitia wizara ya afya imesema inatumia kila mbinu kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Ebola (EVD) uliotangazwa rasmi nchini humo Juni 11 mwaka 2019 baada ya kubaina kwa mtoto wa miaka 5 ambaye ameshafariki dunia pamoja na bibi yake na kaka yake.

Wizara hiyo inasema juhudi zote zilizofanyika za maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa huo sasa ziko katika mtihani na wahudumu wa afya waliojiandaa vilivyo wanachukua tahadhari zote zinazostahili kulinda afya yao nay a umma.

Shirika la afya duniani WHO limesema kila siku timu ya wahudumu wa afya wanakwenda kwenye jamii mbalimbali kujaribu kuzuia kusambaa kwa mlipuko huo ambaopo sasa idadi ya watu walio chini ya uchunguzi na uangalizi kwa siku 21 ili watangazwe kutokuwa na Ebola baada ya kukutana na waathirika imefikia 96.

Hali ya taharuki inaongezeka

Miongoni mwa wana jamii wizara ya afya ya Uganda inasema hamasa , taharuki na matarajio vimeongezeka huku mahitaji ya kupata taarifa na huduma kama chanjo ambayo tayari imeanza kutolewa mishoni mwa wiki vikihitajika zaidi.Akisistiza mambo ya msingi Dkt. Jane Ruth Aceng waziri wa afya wa Ugandaakizungumza na wahudumu wa afya katika wilaya ya Kasese walio msitari wa mbele kuhakikisha wanazuia kusambaa zaidi kwa mlipuko huo  amesema Ebola hivi sasa ni hali halisi katika akili zetu, tunahitaji utulivu wa hali ya juu kwa kila mtu. Mkakati wetu bado unasalia kuwa ni kuzuia, kubaini mapema na kuchukua hatua madhbuti kupambana na ugonjwa huo. Ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika jamii, vituo vya afya na maeneo ya kuinhgilia mipakani ni kipengee muhimu sana cha mkakati wetu ambacho kinatekelezwa kwa nguvu zote baada ya kujutia mtoto wa miaka 5 aliyefariki dunia yeye na familia yake kuweza kukwepa kubainiwa mpkani na kufika katika hospitali ya Kagando.”

Hata hivyo jambo hili si la kushangaza au kutotarajiwa kwani watu katika maeneo haya ya mipakani wanashikamana kwa mambo mbalimbali na wana mahusiano mengine ya damu, biashara, dini, utamaduni au ndoa.

Hatua zingine zilizochukuliwa

Kufuatia dosari hiyo wizara ya afya ya Uganda imesema hivi sasa wajhudumu wa afya wameweka dawati maalum la tahadhari likiorodhesha watu wote waliokutana na mgonjwa huyo wa kwanza Kagando, Bwera na Mpondwe. Pia wanaendesha msako wa visa katika vituo vyote vya afya  ikiwa ni pamoja na kufuatili masuuala ya mazishi katika wilaya hiyo.

Timu ya maabara pia inachangia juhudi zake kwa kuimarisha muda wa kukusanya vipimo , kusafirisha, kupima na kutoa matokeo ili kutoa muongozo wa matibabu na mbinu za kupambana na mlipuko huo.

Mbali ya wahudumu wa afya 4700 wa awali sasa wizara imeongeza wahudumu wengine katika kila wilaya. Naye mwakilishi wa WHO nchini Uganda Dkt. Yonas Tegegn Woldermariam amesisitiza kwamba pointed “uratibu na uongozi imara katika wilaya ni vitu ambavyo vitaonyesha ni haraka kiasi gani mlipuko huu unaweza kudhibitiwa.