Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumkwamua binti wa Kisamburu ni mtihani ninaodhamiria kuushinda: Lerosion

Emily Rosa Lerosion, muasisi wa shirika la kiraia la The New Dawn Pacesetter linalosaidia kunusuru watoto wa kike dhidi ya ndoa za mapema na ukeketaji kwenye jamii ya wasamburu, Kaskazini mwa Kenya
UN News/Patrick Newman
Emily Rosa Lerosion, muasisi wa shirika la kiraia la The New Dawn Pacesetter linalosaidia kunusuru watoto wa kike dhidi ya ndoa za mapema na ukeketaji kwenye jamii ya wasamburu, Kaskazini mwa Kenya

Kumkwamua binti wa Kisamburu ni mtihani ninaodhamiria kuushinda: Lerosion

Wanawake

Mila na desturi katika jamii ya Wasamburu nchi Kenya bado zinamwacha nyuma mtoto wa kike hasa katika masuala ya elimu na kudumisha mila zingine potofu ikiwemo ukeketaji. Hivi sasa wanaharakati mbalimbali kutoka mashirika ya kijamii, kidini na hata serikali wanachukua hatua hususan ya kuelimisha jamii kuhusu thamani na mchango wa  mtoto wa kike katika jamii.

Kuwa msichana katika jamii ya Samburu ni faraja kwa wazazi hasa kina baba ambao wanatarajia kutajirika unapoozwa.  Hiyo ni kauli ya Emily Rosa Lerosion kutoja jamii ya watu wa asili ya Samburu kutoka Kaskazini mwa Kenya anayeshiriki kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa la watu wa asili linaloendelea kwenye makao makuu ya umoja huo mjini New York Marekani. 

Akizungumza nami kandoni mwa jukwaa hilo Emily amesema kwa miaka na mikaka mila ya Samburu inamchukulia msichana kama chanzo cha utajiri ndio maana ndoa za utotoni zinazopingwa vikali na ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs, zimekita mizizi katika jamii hiyo, hali ambayo amedhamiria kuibadili kwa kuanzisha shirika la New Dawn Pacetter ambalo lengo lake kuu ni kuwakwamua wasicha wanaoingozwa kwenye ndoa za utotoni na ukeketaji na kisha kuwarejesha shule. Hiki ni kibarua kigumu Emily anafanje kufanikisha azma yake?

(MAHOJIANO FLORA NDUCHA NA EMILY ROSA LEROSION)