Faida ya kuinuliwa nawe uinuwe wengingine:KPL

15 Machi 2018

Kikao cha 62 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani, washiriki wanaendelea kupigia chepuo juhudi za ukombozi wa wanawake na wasicha wa vijijini kwa kuelezea wanachokifanya. Leo tumekutana na mwanaharakati kutoka nchini Kenya.

Bi Khoboso Hargura Hadichareh ni miongoni mwa wanaharakati hao ni mwanzilishi wa mfuko wa kujitolea uitwao KPL, yaani Kargi Pastroralist Link kwa ajili ya kusaidia jamii ya wafugaji wa kuhamahama wa Rendile kwenye eneo la Marsabit jimbo la Kaskazini Mashariki .

Jamii hiyo inaghubikwa na changamoto lukuki zikiwemo, ukosefu wa maji safi na salama, ufahamu mdogo wa masuala ya ulemavu, masuala ya ukimwi na wanawake kukosa sauti, lakini kubwa zaidi ni tatizo la elimu hasa kwa mtoto wa kike na ndicho kilichomfanya Khoboso kuchukua hatua kwani

(SAUTI YA KHOBOSO ARGURA)

Khoboso HarguraAdichareh/KPL
Mama wa jamii ya rendile akiwa na watoto wake Marsabit Kaskazini Mashariki mwa Kenya, baada ya kupokea msaada wa chakula

Na wito wake ndio huu

(SAUTI YA KHOBOSO  HARGURA)

 

TAGS: CSW62, wanawake, rendile, elimu, KPL, Khoboso Hargura Adichareh

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud