Elimu kuhusu hifadhi ya jamii Tanzania kusaidia kupanua wigo

22 Aprili 2019

Wakati Umoja wa Mataifa ukieleza kuwa upataji wa huduma za hifadhi ya jamii bado ni changamoto kubwa wa wakazi wengi wa dunia, Tanzania imeamua kuchukua hatua madhubuti kwa kutambua kuwa hifadhi  bora ya jamii ni jawabu la siyo tu kupunguza umaskini wa  kaya bali pia umaskini katika ngazi ya taifa.

 

 Tanzania imechukua hatua kuhakikisha hifadhi ya jamii inakuwa na manufaa si tu kwa wafanyakazi walio kwenye sekta rasmi ambao wanachangia mifuko hiyo, bali pia kundi kubwa la watu walio kwenye sekta isiyo rasmi wakiwemo wanawake.

David Kaali ambaye ni Mkurugenzi wa masuala ya hifadhi ya jamii ofisi ya Waziri Mkuu nchini humo, amesema hayo alipohojiwa hivi karibuni na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayotaka hifadhi ya jamii isaidie kuimarisha usawa wa jinsia.

(Sauti ya David Kaali)

Lakini vipi utaratibu kwa mama lishe?

(Sauti ya David Kaali)

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud