Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yachukua hatua ili kila mtu apate maji ifikapo 2030

wanamke akiwa anakwenda kuchota maji katika wilaya ya Chikwawa, Malawi.
Photo: OCHA/Tamara van Vliet
wanamke akiwa anakwenda kuchota maji katika wilaya ya Chikwawa, Malawi.

Tanzania yachukua hatua ili kila mtu apate maji ifikapo 2030

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ikiwa leo ni siku ya maji duniani, maudhui yakiwa hakuna kumwacha mtu nyuma katika kupata huduma hiyo ifikapo mwaka 2030 kwa kuzingatia lengo namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, Tanzania imetaja hatua iliyochukua ili kufanikisha lengo hilo. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. John Jingu, amesema hayo jijini New York, Marekani kandoni mwa mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW, akisema hatua hiyo ni kupitishwa kwa sheria ya mfuko wa maji itakayoondolea adha wanawake na wasichana kusaka maji mwendo mrefu.

(Sauti ya Dkt. John Jingu)

“Maji ni changamoto kubwa. Serikali imepitisha sheria ya mfuko wa maji na  sasa tunao mfuko wa maji na moja ya malengo ya mfuko wa maji ni kuhakikisha kuwa huduma ya maji inafika kila kona ya nchi, inafika mijini na vijijini kila mwananchi aweze kupata huduma ya maji, Niseme kwamba bado hatujakamata nchi nzima lakini maeneo mengi juhudi zinaendelea kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata maji safi na salama.”

Mfuko huo wa maji ulioanzishwa kwa sheria unapata fedha kutoka mauzo ya mafuta ya petrol, dizeli na taa.