Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID wafanikisha msafara wa kutathmini mahitaji huko Darfur kati

Askari wa kikosi cha UNAMID chini ya usimamizi wa Luteni Jenerali Leonard Ngondi, kilichoko UM Baro,kaskazini mwa darfur kikishika doria kijiji cha Basma
Picha na Albert Gonzalez Farran/UNAMID(Maktaba)
Askari wa kikosi cha UNAMID chini ya usimamizi wa Luteni Jenerali Leonard Ngondi, kilichoko UM Baro,kaskazini mwa darfur kikishika doria kijiji cha Basma

UNAMID wafanikisha msafara wa kutathmini mahitaji huko Darfur kati

Amani na Usalama

Walinda amani wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, jimboni Darfur nchini Sudan, UNAMID wamefanikisha misafara ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutathmini mahitaji ya wananchi kwenye kijiji cha Keiling kilichopo kilometa 7 kusini mwa makazi ya muda ya ujumbe huo yaliyopo Golo, Darfur ya kati.

Taarifa ya UNAMID iliyotolewa huko Darfur inasema kuwa mashirika hayo ni yale ya mpango wa chakula duniani, WFP, lile la kuhudumia watoto, UNICEF na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO.

Katika tathmini yao ya pamoja iliyojumuisha pia ujumbe kutoka serikalini, ujumbe huo ulikutana na wawakilishi wa wananchi ambao walielezea wasiwasi wao utokanao na ukosefu wa maji, shule, mbegu za mazao wakati huu wa kuelekea msimu wa kilimo pamoja na ubovu wa barabara kutoka Golo hadi Keiling.

Jukumu la kuhakikisha usalama wa misafara ikiwemo ile ya kupeleka huduma za kibinadamu ni miongoni mwa majukumu ya msingi ya UNAMD kwa upande wa mashirika pamoja na raia.