Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kwa ulimwengu wa Kiarabu kuanza kuishi ndoto zao:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu  Arab League , Tunisia 31 Machi 2019
Screen grab/video of the speech
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Arab League , Tunisia 31 Machi 2019

Ni muhimu kwa ulimwengu wa Kiarabu kuanza kuishi ndoto zao:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuasa ulimwengu wa nchi za Kiarabu kwamba huu ni wakati wa kuanza kuishi kwa kutimiza ndoto zao , kwani eneo hilo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ni eneo lenye mchango umuhimu namkubwa kwa dunia.

Guterres ametoa wito huo leo Jumapili kwenye mkutano wa ngazi ya juu Jumuiya ya nchi za Kiarabu, Arab League unaoendelea mjini Tunis Tunisia akisema lengo lake kuu la kuwa kwenye mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa, mataifa wanachama wa Arab League na watu wa ulimwengu wa Kiarabu. Amesisitiza kuwa “Ni ukanda ambao kwa muda mrefu umekuwa ukihaha kujenga Amani na ustawi bora, na ninaamini ni muhimu kwa ukanda huu kuanza kuishi ndozo hizo. Umoja wa Mataifa hauna ajenda nyingine yoyote Zaidi ya kuunga mkono ndoto hizo kwa lengo la mshikamano na umoja.”

Mchango wa ulimwengu wa Kiarabu

Katibu Mkuu amesema kwa karne na karne dunia imebarikiwa na ubunifu na utamatuni wa Kiarabu, ambao amesema uko bayana katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Sanaa hadi uhandisi, kuanzima madawa hadi hisabati na Filosofia hadi sayansi ya anga za mbali.

Amesisitiza kuwa si historia tu bali pia ameshuhudia ukaribu wa nchi hizo katika kukumbatia wimbi la wakimbizi wakati kwa bahati mbaya mipaka ya nchi nyingi ikiwa imefungwa kwa suala hilo. “Kama Katibu Mkuu nimekuwa nikifanya kazi kwa karibu ili kusongesha mbele jukumu muhimu la ulimwengu wa Kiarabu na jukumu ambalo utaweza kulifanya na ni lazima ulifanye katika wakati wa sasa wa msukusuko.”

Changamoto zilizopo

Katika hotuba hiyo Guterres amesema raia wa nchi za ulimwengu wa Kiarabu wameshuhudia kwa makini picha za kusikitisha na kughadhibisha za vita vya Yemen na Syria , kushamiri na kuporomoka kwa Daesh na kuendelea kunyimwa haki ya kujitawala kwa watu wa Palestina. Hivyo  “Ninatoa wito wa mshikamano wa ulimwengu wa Kiarabu kama msingi muhimu kwa ajili ya amani na mustakabali bora kwenye ukanda mzima na kuepuka kuuacha ukanda huo katika hatari ya kuingiliwa na ushawishi kutoka nje ambao utakuwa na athari za kuyumbisha ukanda huu. Kama ilivyo katika sehemu zingine tunafahamu kwamba maono ya ukanda yanatokana na ushirikiano, heshima na dhamira za pamoja ndivyo vyenye fursa kubwa ya mafanikio.”

Mkutano na waandishi wa habari wa Quartet kuhusu Libya tarehe 31 Machi 2019 mjini Tunis Tunisia. Kutoka kulia Federica Mogherini, mwakilishiwa EU kuhusu mambo ya nje na sera za usalama, Ksatibu Mkuu wa UN Antonio Guterres, Ahmad Abulgheit Katibu mkuu wa m
UN Photo/Ahmed Gaaloul
Mkutano na waandishi wa habari wa Quartet kuhusu Libya tarehe 31 Machi 2019 mjini Tunis Tunisia. Kutoka kulia Federica Mogherini, mwakilishiwa EU kuhusu mambo ya nje na sera za usalama, Ksatibu Mkuu wa UN Antonio Guterres, Ahmad Abulgheit Katibu mkuu wa m

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa juhudi za pamoja zinahitajika zaidi ili kufungua vifungo vya usalama, kutoruhusu machafuko  na kuleta amani, utulivu na serikali ambazo zinawajibika ambazo watu wa ukanda huo wanastahili.

Ameongeza kuwa katika ukanda mzima tunaona ongezeko la madai ya ajira na fursa za kiuchumi , kutekeleza haki za binadamu, kusongesha masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na kuchagiza utawala wa sheria, ujumuishwaji, uhuru wa msingi na maadili ya demokrasia.

Hali halisi ya ukanda mzima

Amesema hivi sasa ukanda mzima una mambo mbalimbali na changamoto zinazoendelea ambazo zinaweza kutatuliwa na kupatiwa ufumbuzi kwa mtazamo madhubuti wa kikanda.

Gaza: Suluhu namba moja ni lazima iwe ya mataifa mawili, kwa Israel na Palestina kuishi pamoja bega kwa bega kwa Amani na kuwa na mipaka inayotambulika na kuufanya mji wa Yerusalem kuwa mji mkuu wa mataifa yote mawili kamanilivyokuwa nikisisitiza kila wakati. “Hakuna mpango mwingine , bila mataifa mawili hakuna sukuhu, mahafuko yanayoendelea Gaza ni zahma inayotukumbusha jinsi hali ilivyo tete.”

Yemen: Kuhusu Yemen Guterres amesema kwa pamoja kuna hatua ambazo zinapigwa ili kuwaondolea madhila watu wa taifa hilo. Ameshukuru pia ukarimu na ahadi zilizotolewa ambapo dola bilioni 2.6 kati ya dola bilioni 4 zinazohitajika zilichangwa ili kuhakikisha operesheni za kibinadamu zinaendelea kwa mwaka 2019. Hata hivyo amesema bado msaada Zaidi unahitajika “Ninatoa wito kwa wahisani wote hapa na kwingineko duniani kutokana na athari za njaa , kipindupindu na madhila yanayoikabili jamii katika wakati huu ambao mashirika ya misaada ya kibinadamu yanakabiliwa na ukata , kuharakisha ahadi zenu mlizotoa ili tuweze kukabiliana na mahitaji ya msingi ya watu wa Yemen.”

Libya: Kuhusu Libya Katibu Mkuu amesema ametiwa moyo na hatua za hivi karibuni kuelekea kuwa na muafaka wa kisiasa kwa kuitisha mkutano wa kitaifa. Ameongeza kuwa ana matumaini kwamba hatua Zaidi zitapigwa kwa kuwa na mchakato unaoongozwa na Walibya wenyewe namchakato wa kisiasa unaomilikiwa na Walibya wenyewe.” Ni wakati sasa wa Libya kufikia kuwa na taasisi za pamoja na kuhitimisha hatua ya mpito kwa kuzingatia lengo la kufikia kwa wakati muafaka  la kuwa na uchaguzi mkuu.”

Syria: Katibu Mkuu amesema nchini Syria mamilioni ya Wasyria bado wametawanywa na machafuko, maelfu wanashikiliwa na hatari ya zahima kubwa ya kibinadamu bado inanyemelea hususan Kaskazini mwa Syria. Amehimiza juhudi zaidi za kupata suluhu ya kisisa kama njia ya kuelekea Amani ya kudumu ambayo itawapa sauti Wasyria wote, kushughulikia machungu yao na kutimiza mahitaji yao. “Suluhu yoyote ya mgogoro wa Syria lazima ihakikishe kunakuwa na umoja, hadhi ya taifa la Syria ikiwemo eneo linalokaliwa na Golani kwa hili msaada kamilifu wa jumuiya ya kimataifa na hususan Jumuiya ya nchi za Kiarabu na wanchama wake ni muhimu.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres
UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Ugaidi: Kuhusu vita dhidi ya ugaidi Guterres amesema ukanda wa nchi za Kiarabu na watu wake wamejitolea kwa kiasi kikubwa kupambana na ugaidi na wamelipa gharama kubwa katika hilo na kwamba “Umoja wa Mataifa unaongeza msaada kwa mataifa ya Kiarabu katika vita hivi ikiwemo kupitia makubaliano ya kuanzishwa mkakati wa ukanda wa Kiarabu wa kukabiliana na ugaidi kwa kuzingatia matakwa ya Umoja wa Mataifa. Juhudi hizi na zingine kutoka mataifa ya Kiarabu zitasaidia kufungua mlango kwa suluhu ya Kiarabu na matatizo ya nchi za Kiarabu.”

Lebanon:Kuhusu Lebanon Katubu Mkuu amesema kuundwa kwa serikali mwezi Januari kunatoa fursa muhimu ya kushughulikia changamoto za utulivu kwa kuzingatia mpango wa 2018 wa mikutano ya kimataifa ya msaada kwa ajili ya faida ya taifa zima.

Algeria:Katibu Mkuu amekaribisha juhudi za mchakato wa kuelekea kipindi cha mpito cha Amani na demokrasia ili kushughulikia hofu za watu wa Algeria kwawakati muafaka.

Somalia: Amesema kwa Somalia ni muhimu kutambua hatua zilizopigwa katika mchakato wa kufufua na kuimarisha uchumi na kushikamana kwa ajili ya juhudi za taifa hilo na kazi ya pamoja ya kuchagiza majadiliano jumuishi ya kisiasa na kuwekeza katika ufufuaji uchumi wa Somalia.

Amewashukuru wote kwa mchango wao mkubwa kwa Umoja wa Mataifa ambao amesema ni nyenzo muhimu katika kutatua migogoro na kusaka Amani ya kudumu kote duniani.”Hebu tufanye kazi kwa karibu ili kuibua umuhimu wa ukanda huu, kutekeleza matakwa ya vijana na kujenga mustakabali bora kwa wote.”