Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji ni uhai unaolinda afya na mazingira:Guterres

Siku ya maji duniani
UN
Siku ya maji duniani

Maji ni uhai unaolinda afya na mazingira:Guterres

Haki za binadamu

Maji ni muhimu sana kwa uhai wa mtu sanjari na usafi vinasaidia kulinda afya ya jamii na mazingira. Amesema hayo hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya maji duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Machi 22.

Guterres amesema “miili yetu, miji yetu, viwanda vyetu, kilimo chetu na mifumo yetu yote ya maisha inategea maji. Maji ni haki ya binadamu na haipaswi yeoyote kunyimwa haki hiyo na maadhimisho ya siku hii ni katika kuzingatoia haki hiyo kwa wote na kutomuacha yeyote nyuma”.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa leo hii watu bilioni 2.1 wanaishi bila maji safi kwa sababu kama za kuchumi, jinsia, asili yao, dini na umri. Ongezeko la mahitaji pamoja na udhibiti mbovu vimeongeza shinikizo la maji katika sehemu nyingi duniani huku akisema mabadiliko ya tabiacnhi nayo yameongeza shinikizo.

Kwa mujibu wa ujumbe huo ifikapo mwaka 2030 inakadiriwa kuwa watu milioni 700 watatawanywa kote duniani kutokana na upungufu mkubwa wa maji.Ujumbe huo umechagiza ni lazima kuwepo ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za maji duniani na kuimarisha mnepo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha kwamba kuna fursa ya maji kwa wote  na hususan kwa walio hatarini zaidi.

Guterres amesisitiza kuwa hatua hizi ni muhimu katika kuelekea mustakbali wa amani na utulivu wenye mafanikio, kwani wakati dunia ikipambana kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs ni lazima pia kuthamini rasilimali ya maji na kuhakikisha udhibiti wake ni jumuishi endapo tunataka kulinda na kutumia rasilimali hii kwa njia endelevu na kwa faida ya watu wote.