Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simanzi na rambirambi vyaendelea kutawala UN

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa jijini Nairobi walkati wa dakika moja ya ukimwa kuwakumbuka watu waliofariki kwenye ajali ya ndege ya Ethiopia Machi 11, 2019
UN Nairobi/Tirus Wainaina
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa jijini Nairobi walkati wa dakika moja ya ukimwa kuwakumbuka watu waliofariki kwenye ajali ya ndege ya Ethiopia Machi 11, 2019

Simanzi na rambirambi vyaendelea kutawala UN

Masuala ya UM

Simanzi hali ya mshituko na rambirambi vimeendelea kumiminika na kutawaka kwenye Umoja wa Mataifa kufuatia msima mkubwa kwa kuondokewa na wafanyakazi wake 21 kwenye ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ambayo kwa ujumla imekatili maisha ya watu 157 mwishoni mwa wiki 

Rais wa Baraza Kuu la UN Maria Fernanda Espinosa

Wafanyakazi na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Mataifa na mashirika yake wamekuwa wakielezea hisia zao kuhusu msiba huu mkubwa. Rais wa Baraza Kuu Maria Fernanda Espinisa akiandika kwenye ukurasa wake wa twitter amesema “ rambiramboi zangu za dhati ziwaendee familia na marafiki wote wa waliopoteza maisha , hii ni safari mashuhuri kwa wote wanaopigania mema kwa bara la Afrika na mawazo na fikra zangu ziko na wote walioathirika kwa njia moja au nyingine na ajali hii mbaya kabisa ya shirika la ndege la Ethiopia.”

Michael Møller mkurugenzi mkuu wa UNOG

Mjini Geneva Uswisi pia salamu za rambirambi zimetumwa na mkurugenzi mkuu wa osfisi ya Umoja wa Mataifa (UNOG) akielezea kushitushwa sana na ajali hiyo ya ghafla iliyoacha majonzi “Nimeshitushwa sana na ajali hii mbaya kabisa kwa familia ya Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla. Ameongeza kuwa kwenye ndege hiyo kulikuwa pia na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha ambao walikuwa safarini kuelekea Nairobi kutoka mashirika balimbali ya Umoja wa Mataifa Geneneva.

WFP imepoteza wafanyakazi 7 katika ajali hiyo

Miongoni mwa mashirika ya umoja wa Mataifa yaliyopoteza wafanyakazi wake kwenye ajali hiyo ya Jumapili ni shirika la mpango wa chakula duniani WFP, ambalo mkurugenzi wake mtendaji amesema “kila mmoja wa wafanyakazi hao alikuwa tayari kusafiri na kufanya kazi mbali na nyumbani watokako na wapendwa wao ili kusaidia kuifanya dunia hii kuwa mahala bora pa kuishi.”

Wafanyakazi wenzetu watatu wametuacha-UNHCR

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakipimbizi UNHCR lipo katika maombolezo ya kuondokewa na wafanyakazi wake watatu katika ajali hiyo ya ndege ET 302 iliyokuwa ikitokea Addis Ababa Ethiopia kuelekea Nairobi Kenya jana asubuhi na kuangua dakika sita tuu baada ya kupaa. Wafanyakazi hao ni Nadia Ali, Jessica Hyba na Jackson Musoni.

Kamishina Mkuu wa wakimbizi Fillipo Grandi akikatisha ziara yake Mashariki ya Kati na kurejea makao makuu ya UNHCR Geneva, kwa uchungu amesema “Tumekumbwa na pigo kubwa na la ghafla , hili ni janga kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo sala na dua zetu ziko pamoja nao.”

Na kwa familia hizo amewaahidi “ Tunafanya kila tuwezalo kuzisaidia familia za Nadia, Jessica na Jackson katika wakati huu mgumu wa majonzi na uchungu mkubwa, na kwa niaba ya wafanyakazi wote wa UNHCR duniani natuma rambirambi zangu za dhati , kwani leo tunawaomboleza wafanyakazi wenzetu na marafiki zetu wa karibu. UNHCR imepoteza wahudumu wa kibinadamu waliojitolea bila kuchoka kwa ajili ya mamilioni ya watu waliolazimika kufungasha virago na kukimbia vita na mateso kote duniani.”