Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani vikali tukio la kigaidi mjini Bogota Colombia.

Picha kutoka juu ya mji wa Bogotá, Colombia.
World Bank/Dominic Chavez
Picha kutoka juu ya mji wa Bogotá, Colombia.

Umoja wa Mataifa walaani vikali tukio la kigaidi mjini Bogota Colombia.

Amani na Usalama

Katiku Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la bomu katika chuo cha polisi mjini Bogota nchini Colombia. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stéphane Dujarric jijini New York, Marekani, Guterres ametuma pia salamu zake za rambirambi kwa familia za waathirika wa shambulio hilo la jana Alhamisi na akawatakia ahueni ya haraka wote waliojeruhiwa katika tukio hilo la bomu lililotegwa katika gari na kusababisha vifo vya takribani watu 21 na makumi walijeruhiwa.

Mamlaka za Colombia zimeonesha kuwa zina uthibitisho kuwa tukio hili la kigaidi limetekelezwa na kundi la National Liberation Army (ELN) na kwa hivyo Katibu Mkuu ametoa wito kuwa wahusika wote wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

“Katibu Mkuu anaungana na watu na serikali ya Colombia katika kipindi hiki cha majonzi” imesema taarifa hiyo.

  Naye rais wa Baraza wa Kuu la Umoja wa Mataifa María Fernanda Espinosa mapema jana kupitia ukurasa wake wa Twitter alilaani tukio hilo na kuwatakia ahueni ya haraka wote waliojeruhiwa katika tukio hilo.

 

Tweet URL