Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Maria Fernanda Espinosa kupitia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya sayari Dunia yaliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani hii leo, ametoa tahadhari kuwa “dunia yetu iko katika hatari kubwa na sasa ni wakati wa kuijali sayari hii.”