Baada ya kusuasua WHO na wadau wazindua kampeni mpya ya kutokomeza Malaria.
Kasi ya kupunguza visa vya malaria imesimama baada ya miaka mingi ya kupungua kwa visa hivyo kote duniani, kwa mujibu wa ripoti mpya ya malaria duniani 2018 iliyotolewa leo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa na shirika la afya ulimwenguni, WHO wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na Malaria itakayosaidia kurejesha kasi ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo, vifo vitokanavyo na malaria na kasi ya mapambano katika mstari unaostahili jitihada kubwa zinapaswa kufanyika katika uzuiaji n atiba, lakini pia uwekezaji ili kuwalinda watu walio katika hatari ya kupata maradhi hayo.
Ripoti imetaja sababu za kupungua kwa kasi ya kudhibiti visa vipya vya malaria kuwa ni pamoja na watu wengi barani Afrika kutotumia vyandarua vyenye viuatilifu wanapolala, nyumba kunyunyuziwa dawa za kuua mbu kama ilivyokuwa awali na wajawazito kutopatiwa kwa kiasi cha kutosha huduma za kujinga na malaria.
Dkt Kesete Admasu Mwandamizi Mkuu wa ushirika wa RBM-Role back Malaria.akieleza kuhusu mkakati huo uliopewa jina “mzigo mkubwa na kishindo kikubwa” amesema unajikitakatika masuala manne muhimu.Kampeni hii ina misingi muhimu minne:kuamsha uhamasishaji wa kitaifa na kimataifa ili kupunguza vifo vitokanavyo na malaria; kuweka msukumo kupitia matumizi ya kimkakati ya taarifa; kuweka mwongozo, sera na mikakati ambayo inaendana na mataifa yote yanayosumbuliwa na malaria na pia utekelezaji wa mwitikio wa kitaifa ulioratibiwa.Lakini la msingi zaidi ni“Nguzo ya kwanmza ni utashi wa kisiasa, ili kuwezekza katika malaria,. Na pia kuhakikisha kuwa kuna azma mpya ya uongozi wa kitaifa katika mataifa yanayohusika. Bila utashi wa kisiasa itakuwa vigmu kufanikisha malengo yetu ya pamoja.”
Lengo kuu la mkakati huu amesema ni kupunguza vifo vya malaria kwa takriban asilimia 40 ifikapo mwaka wa 2020. Kwa mwaka wa pili mfululizo ripoti ya WHO imeonyesha kuwa idadi ya wanaoathirika na malariainaongezeka. Mfano mwaka 2017 ilikadiriwa kuwepo visa vya malaria milioni 219 ilikilinganishwa na visa milioni 217 mwaka 2016.
Mwaka 2017 kulikuwa na takriban asilimia 70 ya visa malaria sawa na watu milioni 151 na vifo 274,000 vilitokea katika mataifa 10 ya Afrika na Asia. Barani Afrika mataifa hayo ni pamoja na Uganda na Tanzania , Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC, -Niger, Nigeria, Ghana, Mali, Burkina Faso, na Cameroon.