Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mafanikio sasa kuna hofu kuhusu Malaria- Ripoti

Kulala ndani ya chandarua chenye kiuatilifu huleta nuru na matumaini kwa afya ya mtoto. (Picha:UNfoundationblog)

Licha ya mafanikio sasa kuna hofu kuhusu Malaria- Ripoti

Idadi ya wagonjwa wa Malaria kwa mwaka 2016 iliongezeka kwa zaidi ya visa milioni 5 ikilinganishwa na mwaka 2015 na hivyo kutiwa hofu juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kutokomeza ugonjwa huo.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la afya ulimwenguni, WHO iliyotolewa Jumanne ikiongeza kuwa hata idadi ya vifo vitokanavyo na Malaria vimesalia 445,000 ikiwa ni sawa na mwaka 2015.

WHO inasema kwa hali ilivyo sasa, dunia iko njiapanda na ni lazima hatua ichukuliwe ili kuepusha kurejea katika hali ya zamani na hivyo kushindwa kufikia lengo la kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030.

image
Mama na mwanae wakiwa na matumaini baada ya kupata chandarua. (Picha:Unfoundationblog)
Moja ya sababu iliyotajwa katika mkwamo wa kudhibiti Malaria ni upungufu wa ufadhili ambapo tatizo kubwa ni kupata fedha kutoka vyanzo vya ndani ya nchi na hata kimataifa ili kununua vyandarua vyenye viuatilifu, dawa na vifaa vingine vya kukabiliana na Malaria.

Akizungumzia kutokupungua kwa visa vya Malaria, Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho, ambaye ni mwenyekiti wa ubia wa kutokomeza Malaria duniani, RBM ameieleza idhaa hii kuwa.

(Sauti ya Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho)

Na hivyo Dkt. Winnie anapendekeza ufadhili wa kifedha lakini ..

 (Sauti ya Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho)

image
Mgao wa vyandarua kwa watoto huko Sudan Kusini. (picha:UNfoundationblog)