Wakati wa mkutano mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa mwaka huu, viongozi wa dunia, wadau wa afya na wawakilishi wa jamii wanaungana na shirika la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID, kutoa wito wa upatikanaji wa haraka na usawa zaidi wa bidhaa za afya zinazookoa maisha ili kuendeleza mchakato wa kupambana na changamoto kubwa zaidi za leo za afya, ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi ya mama na mtoto, kuzuia majanga, kujiandaa na hatyua za kukabiliana na majanga, na virusi vya ukimwi VVU, kifua kikuu na malaria.