Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuondolewa kwa vikwazo dhidi  ya Eritrea kutachagiza ujenzi wa amani- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Kuondolewa kwa vikwazo dhidi  ya Eritrea kutachagiza ujenzi wa amani- Guterres

Amani na Usalama

Kufuatia hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Eritrea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema anafuatia kwa karibu maendeleo ya sasa huko Pembe ya Afrika akisema ni matumaini yake kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutachangia katika kusongesha juhudi za amani kwenye eneo hilo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Bwana Guterres amesema hatua hiyo pia itaimarisha mazingira bora kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi kwenye ukanda huo sambamba na maendeleo endelevu.

Bwana Guterres amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake uko tayari kusaidia nchi za ukanda wa Pembe ya Afrika katika kushughulikia changamoto zilizosalia za amani na usalama.

“Umoja wa  Mataifa pia uko tayari kusaidia mazungumzo yanayoendelea kati ya Djibouti na Eritrea pamoja na juhudi za kikanda za kumaliza masuala yaliyosalia kati ya nchi mbili hizo,” imemalizia taarifa hiyo ikimnukuu Katibu Mkuu.